LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu Majaliwa awapa pole watanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaaliwa amesema ajali za barabarani zimekuwa chanzo cha kinachogharimu maisha ya wananchi wakiwemo watumishi wa umma na binafsi na kutoa maagizo 13 kwa Baraza la Usalama Barabarani nchini ikiwemo kuboresha Sheria ya Usalama Barabarani ili kusaidia kupambana na ajali hizo.

Majaliwa ameyasema hayo Machi 14, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuanzia Januari 2020 hadi Disemba 2022 ajali za barabarani zilisababish vifo vya abiria 1,582 huku majeruhi wakiwa ni 4,372.

Alisema katika kipindi hizo, watembea kwa miguu 958 wapoteza maisha kwa kupitiwa na magari huku 650 wakijeruhiwa.

Majaliwa alibainisha kuwa watumia bodaboda wakiwemo abiria na madereva 797 walifariki huku 725 wakijeruhiwa. Alisema jumla ya waendesha baiskeli 196 waliopoteza maisha na wengine 82 wakijeruhiwa. Katika kipindi hicho, madereva pekee walifariki ni 509 huku 584 wakijeruhiwa.

Majaliwa alisema wajasiriamali watembeleza mikokoteni nao walipata athari za ajali ambapo watu 17 waliopoteza maisha huku 14 wakijeruhiwa.

Kwa takwimu zote hizo, Majaliwa alisema jumla ya ajali zilizotokea katika kipindi hicho cha miaka mitatu ni 5,132. Vifo jumla ni 4,060 na majeruhi 6,427.

"Idadi hii ya vifo na majeruhi kutokana na ajali ni kubwa mno. Nawasihi watanzania tutafakari kwa kutii sheria za usalama barabarani na hapo tutaweza kuziepuka" alisisitiza Majaliwa na kuongeza;

"Niungane na Sagini (Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini) kuwatakia pole waliopoteza wapendwa wao na kuwaombea majeruhi wapone haraka".

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini alisema ajali nyingi zinazotokea barabarani zinatokana na makosa ya kibinadamu ikiwemo mwendo kasi, ulevi, kutofunga mikanda, watumiaji bodaboda na watumiaji barabara kutotii sheria.

"Uchunguzi unaonyesha watumiaji wa mabasi ya mikoani yanayosafiri umbali mrefu ikiwemo Mwanza-Dodoma- Dar ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajali barabarani, kwa sababu hatufuati Kanuni za kuwa na madereva wawili ili kutoa fursa kwa madera kupumzika. Dereva mmoja kuendesha hadi Dar ni uzembe na haikubaliki" alisema Sagini na kuongeza;

"Niwaagize askari kuhakikisha makampuni ya usafirishaji yanakuwa na madereva zaidi ya mmoja kwa safari za umbali mrefu".

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima alisema lengo la maadhimisho hayo ni kukumbushana matumizi sahihi ya usalama barabarani ili kuepusha ajali. Alisema elimu ikiwemo kuepuka mwendo kasi, ulevi na uvaaji kofia ngumu kwa bodaboda itasaidia kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha uharibifu wa mali, mauti na ulevu kwa wananchi.

Malima alisema kila mtumiaji wa barabara ana wajibu wa kuhakikisha anapambana na kuzuia ajali za barabarani ili kuendana na kaulimbiu ya maadhimisho hayo isemayo "Tanzania bila ajali inawezekana, timiza wajibu wako".

Akitoa takwimu za ajali kwa kipindi cha mwaka 2022, Malima alisema ajali 81 za barabarani ziliripotiwa mkoani Mwanza ambazo zilisababisha vifo 71, majeruhi 96. Alisema ajali za bodaboda zilikuwa 30 zilizosababisha vifo 25 na majeruhi 26. "Nawataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria ili kupunguza idadi hii ya ajali zinazosababisha vifo na majeruhi" Malima.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura alisema "sote ni wahanga wa barabara hivyo tunao wajibu wa kuhakikisha tunazingatia matumizi sahihi. Tunaendelea kutoa elimu kwani ndio chanzo cha kujikinga na ajali ambazo zimekuwa zinagharimu maisha ya watu".

"Mbali na elimu, bado tunaendelea kuchunguza kiini cha ajali za barabarani. Awali wananchi na watafiti walilalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara lakini sote tunauona jinsi Serikali imeendelea kuboresha mtandao wa barabara lakini bado ajali zinatokea" alisema IGP. Wambura.

Katibu Mtendaji Baraza la Usalama Barabarani nchini, SACP. Ramadhan Ng'anzi alisema katika kipindi cha maadhimisho hayo, baraza hilo limeandaa mafunzo kwa viongozi wa bodaboda, waalimu wa somo la usalama na kuchunguza ubora wa vyombo vya barabarani pamoja na kupima afya za madereva ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ajali za barabarani kwani uchunguzi unaonyesha asilimia 80 ya ajali hizo husanabisja na makosa ya kibinadamu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani 2023 kitaifa jijini Mwanza.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaaliwa akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Fuatilia picha mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.