LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO Mwanza washiriki Wiki ya Usalama Barabarani 2023

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza limeshiriki maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kuanzia tarehe 14-17 Machi 2023.

Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga amesema Shirika hilo limetumia fursa ya maadhimisho hayo kwa kuungana na wadau wa usalama barabarani ikiwemo Jeshi la Polisi kuwahimiza watumiaji wa barabara hususani vyombo vya moto kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo zilizo kando kando ya barabara.

Kayaga amesema ajali za barabarani zimekuwa zikilisababishia Shirika la TANESCO hasara kubwa ya kubadilisha miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo baada ya kugongwa na magari, na pia kukosekana huduma ya umeme kwa muda na kusababisha adha wateja.

Ameongeza kuwa pia Shirika la TANESCO ni mdau mkubwa wa usafirishaji ambapo pia lina kada ya madereva hivyo limetumia fursa ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kuwahimiza madereva wake kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani ili kufanikisha shughuli za Shirika kwa weledi.

Naye Shaban Mbialo kutoka Idara ya Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa Mwanza amesema wamepata elimu ya usalama wa umeme, utunzaji wa miundombinu ya umeme na huduma ya kisasa ya Ni-Konekt ambayo inamwezesha mteja kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kidigijali na kuondokana na adha ya kufika ofisini.

"Ni-Konekt ni mfumo rahisi wa maombi ya huduma ya umeme kwa njia ya mtandao ambayo inamwezesha mteja kupata huduma bila kufika katika ofisi za TANESCO ambapo mfumo huu unatumia njia tatu ambazo ni tovuti ya TANESCO www.tanesco.co.tz, kupiga nambari *152*00# na aplikesheni ya NiKonekt" amesema Mbialo.

Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la TANESCO kwenye maadhimisho hayo akiwemo Mzee Khalifa Noti ameeleza kunufaika na elimu ya usalama wa umeme, dalili zinazoweza kuhatarisha vifaa vya umeme na kutoa taarifa mapema kwa wataalamu wa umeme anapobaini hitilamu katika mfumo umeme.

Akizungumza baada ya kutembelea banda la TANESCO kwenye maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Adam Malima ametoa pongezi kwa Shirika hilo kwa jitihada zake za kuhakikisha usalama mahala pa kazi ambazo zinasaidia kupambana na majanga mbalimbali ikiwemo ajali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (kushoto) akipata ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na TANESCO ikiwemo usalama mahala pa kazi kutoka kwa Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (katikati).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima (kushoto) akipata ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na TANESCO ikiwemo usalama mahala pa kazi kutoka kwa Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia).
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda ya shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda ya shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda ya shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Shaban Mbialo (kushoto) kutoka Idara ya Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wananchi kuhusiana na huduma zinazotolewa na shirika hilo.
Shaban Mbialo (wa pili kushoto) kutoka Idara ya Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wananchi kuhusiana na huduma zinazotolewa na shirika hilo.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) akimwelekeza mmoja wa wananchi waliofika katika banda la shirika hilo kuhusiana na huduma ya kidijitali ya NiKonekt.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda ya shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani kitaifa jijini Mwanza.
Jiulize "ikiwa mdoli unafahamu umuhimu wa usalama, sisi ni nani tusizingatie usalama?🤣

No comments:

Powered by Blogger.