LIVE STREAM ADS

Header Ads

Manispaa ya Singida kuiandikia barua NDC, Tanesco kwa kutelekeza mradi wa umeme jua

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu, akiongoza kikao cha kawaida cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2020/ 2023 cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi May 11, 2023.


Na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imeazimia kuliandikia barua Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ili kama yameshindwa kuendeleza eneo la hekta 500 walilochukua kwa miaka zaidi ya 10 kwa ajili ya uwekeza mradi wa umeme wa jua walirudishe kwa manispaa.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, alisema hayo kwenye kikao cha kawaida cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2020/ 2023 cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoketi May 11, 2023.

“Kwakuwa manispaa ndio ilitoe eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji huo kwa hiyo tutawaandikia barua hayo mashirika ili kama wameshindwa kuwekeza waturudishie tutafute mwekezaji mwingine,” alisema.

Hatua ya Mkurugenzi kueleza hayo ilifuatia baada ya Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama kuiomba manispaa hiyo kuwasiliana na Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) ili liweze kurudisha eneo la hekta 500 walilolichukua kwa ajili ya kuwekeza mradi wa umeme wa jua ambalo kwa zaidi ya miaka 10 eneo hilo halijafanyiwa uwekezaji wowote.

"Mheshimiwa Meya eneo hilo ni la wananchi ambao walilitoa kwa ajili ya kupisha uwekezaji ambao ungefanywa kwa ubia kati ya NDC na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tangu mwaka 2012 lakini hadi leo hii hakuna uwekezaji wowote uliofanyika"alisema Mdama.

Mdama alisema eneo hilo lipo Kata ya Unyianga B na lilitengwa kwa ajili ya uwekezaji lakini kwa kuwa limekuwepo kwa muda mrefu bila kuendelezwa anaomba lirudishwe kwa wananchi hili waweze kulitumia kwa kilimo na ufugaji.

Aidha, Mdama alisema kama atatokea mwekezaji mwingine apewe eneo hilo kwani akiwekeza Serikali itapata fedha kutokana na kodi na wananchi watanufaika kwa kulipwa fidia ambayo hawakupewa wakati likichuliwa na NDC.

Katika hatua nyingine madiwani wa manispaa hiyo wameomba kupatiwa semina ili waweze kuzijua shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambazo wamedai hawazijui vizuri.

Hoja hiyo ilikuja baada ya Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Mrua kuzungumzia changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa kata yake waliopo kwenye mfuko huo zikiwemo za kutolipwa fedha zao ambapo aliomba kupatiwa majibu kwenye kikao hicho

"Sisi madiwani tumekuwa na changamoto kubwa ya kujibu maswali ya wananchi wetu ambao wapo katika mfuko huu wa TASAF hasa pale wanapotuletea malalamiko ya kutolipwa fedha baada ya kufanya kazi, kuondolewa katika mpango na ukomo wa umri wa mtu kuwa ndani ya mpango wa mfuko huo na wale ambao wanaondolewa," alisema Diwani wa Kata ya Kisaki, Moses Ikaku.

Diwani wa Viti Maalum, Margaret Malecela aliwataka wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ukimwi kuacha kusubiri vikao vya baraza hilo ili kutoa taarifa badala yake watoke kwenda kuhamasisha jamii ichukue tahadhari ya ugonjwa huo jambo litakalo saidia kupunguza maambukizi.

“Hali sio nzuri maambukizi ya VVU kwa wanawake ni makubwa sana kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba hadi Disemba ulifanyika upimaji wa VVU jumla ya wanaume waliopima walikuwa ni 2,801 na waliokutwa na VVU ni 51 na wanawake waliopima walikuwa 4,399 waliokuwa na VVU ni 228 huku jumla ya waliopima ni 7,200 na waliokutwa na VVU ni 279 sawa na asilimia 18,” alisema Malecela.

Meya wa Manispaa hiyo Yagi Kiaratu alisema katika kipindi hicho cha robo ya tatu Januari hadi Machi mapato waliyopata ni asilimia 88 kwa mapato huru na kwa mapato fungwa walirudi nyuma na kufikia asilimia 73 kutokana na watu wachache waliojitokeza kujiunga na mfuko wa bima ya afya wa CHF iliyoboreshwa.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao hicho
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe akizungumza kwenye kikao hicho.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lusia Mwiru, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe na Katibu wa CCM Wilaya ya Singida, Shabani Hamisi.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Mwankoko, Emmanuel Emadaki, akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Mtamaa, Gwae Mbua akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Kisaki, Moses Ikaku akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Uhamaka, Senge Senge akichangiajambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Mrua akichangia jambo.
Waratibu wa vikao wa Manispaa ya Singida wakiwajibika wakatiwa kikao hicho.
Madiwani Valerian Kimambo (kuhoto) wa Kata ya Mughanga na Hamisi Baraka wa Kata ya Mandewa wakipitia kabrasha wakati wa kikao hicho.
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Dk.Hamis Yuna akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama akichangiajambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalum, Anisa Awadhi akichangia jambo. Kulia ni Diwani Viti Maalum, Saidat Mziray.
Diwani wa Viti Maalum, Margareth Malecela akichangijambo kuhusu VVU na Ukimwi.
Afisa Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dk.Chijo Matekere akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na namna ya kujiunga.
Diwani wa Viti Maalum, Hadija Simba akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Mandewa, Hamisi Baraka, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.

No comments:

Powered by Blogger.