LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ilemela yafanya vizuri utoaji lishe mashuleni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Jumla ya shule 52 kati ya 76 za serikali zilizopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza zimeanza kutoa lishe shuleni ili kuboresha afya za wanafunzi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa divisheni ya elimu ya msingi na awali Mwamu Busungu wakati akiwasilisha taarifa ya utoaji chakula kwa shule za msingi za wilaya ya Ilemela mbele ya wajumbe wa kamati ya lishe.

Mwamu amesema mpango uliopo ni kuhakikisha hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei shule zote zinatoa lishe kwa wanafunzi wa kuanzia darasa ya awali hadi darasa la saba na kuhakikisha kuwa chakula kitakachotolewa kina virutubishi vitakavyo boresha afya za wanafunzi.

‘Lazima tuhakikishe chakula wanachokula watoto wetu hasa wa madarasa haya ya awali kinakuwa na virutubishi kwa sababu watoto hawa wanatakiwa kuimarika kimwili na kiakili ili waweze kuwa bora hapo baadae’.alisema Mwamu

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shunguli za lishe ,Ofisa lishe Paulina Machango amesema katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 Januari – Machi baadhi ya shughuli zilizotolewa ni pamoja na kutoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi wa kata za Bugongwa,Ilemela na Nyamh’ongolo.
Shughuli zingine ni uhakiki wa ubora wa takwimu za viashiria vya lishe kwa vituo vya kutolea huduma ya afya na mama na mtoto,Ununuzi wa chakula dawa kwaajili ya kutibu watoto wenye umri chini ya miaka 5 wenye Utapiamlo pamoja na shughuli nyingine.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya lishe halmashauri ya manispaa ya Ilemela wamesisitiza juhudi zaidi zifanyikeza kuhakikisha shule zote zinatekeleza mpango wa chakula shuleni.

Mbali na hayo wameitaka halmashauri kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu utoaji wa chakula katika shule zote za msingi na sekondari kwa kuhakikisha unafanyika

Sanjari na hayo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri ya manispaa yaIlemela kupitia idara ya afya imetenga kiasi cha milioni 85.8 kutoka mapato ya ndani kwaajili ya utekelezaji wa shuguli za lishe.

Hii ni kulingana na idadi ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwaajili ya kutekeleza shughuli za lishe na hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 77.5
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imetamka wazi kuwa utoaji wa huduma muhimu kama chakula bora, maji safi na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanafunzi wawapo shuleni ni muhimu.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.