LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbio za Mabaharia 2023 zafana jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wamiliki wa vyombo vya usafiri majini wamehimizwa kuweka nyenzo za kufanyia mazoezi katika mazingira ya kazi ili kuwawezesha mabaharia kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha afya zao.

Rai hiyo imetolewa Juni 25, 2025 na Kamanda (CDR) wa kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame wakati akihitimisha mbio za hisani za mabaharia (Seafarers Marathon 2023) zilizofanyika jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani.

CDR. Makame amesema mazoezi yanaimarisha afya hivyo mabaharia ambao hutumia muda mwingi wakiwa kazini wakiwekea miundombinu ya kufanya mazoezi itaimarisha afya zao na kuongeza ufanisi zaidi kazini.

“Nitoe rai kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri majini kuwa na nyenzo za kufanyia mazoezi kwenye meli, hii itahamasisha mabaharia kufanya mazoezi” amesema CDR. Makame na kuongeza kuwa mbio hizo zimesaidia kuwaweka mabaharia pamoja ili kufahamiana na kuimarisha mahusiano kazini.

Baadhi ya washiriki akiwemo Evarist Gimanwa aliyeibuka mshindi wa kwanza wamesema mbio hizo zimesaidia kuhamasisha mabaharia kufanya mazoezi pamoja na kufikisha ujumbe kwa jamii kutambua mchango mkubwa wa mabahari nchini

Maashimisho ya siku ya mabaharia duniani yalianza Juni 22, 2023 katika uwanja wa Furahisha yakiambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji elimu kwa jamii, kufanya usafi katika fukwe za Ziwa Victoria ambapo kilele chake ni Juni 25, 203.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Kamanda (CDR) wa kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame akizungumza wakati wa kuhitimisha mbio za mabaharia (Seafarers Marathon) zilizofanyika jijini Mwanza, jumapili Juni 25, 2023.
Kamanda (CDR) kutoka kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame (kushoto) akimkabidhi medali mshindi wa kwanza wa mbio za mabaharia, Evarist Gimanwa (kulia).
Mbio za mabaharia zimelenga kuimarisha afya, kuwaweka mabaharia pamoja na kutunza mazingira kwa manufaa ya shughuli za majini.
Kamanda (CDR) kutoka kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame (kushoto) akimkabidhi medali mshindi wa pili wa mbio za mabaharia, Jusitus Salvatory (kulia).
Kamanda (CDR) kutoka kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame (kushoto) akimkabidhi medali mshindi wa tatu wa mbio za mabaharia, Andrew Limbu (kulia).
Kamanda (CDR) kutoka kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame (kushoto) akimkabidhi medali mshiriki wa mbio za mabaharia, Mwanakombo Vuai (kulia).
Washiriki mbalimbali wakiwemo mabaharia wakipokea medali baada ya kushiriki mbio za mabaharia 2023 jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimu ya Siku ya Mabaharia Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023.
Mgeni rasmi, Kamanda (CDR) kutoka kikosi cha KMKM Zanzibar, Hussein Makame (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mbio za mabaharia zilizofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mbio za mabaharia 2023 wakiwa uwanja wa Furahisha kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani.

No comments:

Powered by Blogger.