LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zumaridi aandaa hafla kubwa ya kumshukuru Mungu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wafuasi wa Mhubiri Diana Bundala maarufu Mfalume Zumaridi wamemuandalia sherehe ya kumshukuru Mungu baada ya kutoka gerezani ambapo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne Juni 27, 2023 Mfalme Zumaridi alisema wafuasi wake wameandaa sherehe hiyo kumshukuru Mungu kwa kumsaidia kutoka gerezani.

Alisema sherehe hiyo itafanyika Julai 08, 2023 nyumbani kwake Mtaa wa Bugugu uliopo katika Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana ambapo itahudhuriwa na zaidi ya watu 2,000.

"Nimekaa kwa muda mrefu bila kuongea na waandishi wa habari, nimewaita ili kuzungumza nanyi kuelekea kwenye sherehe hii kubwa ya Shukurani kwa Mungu wangu aliyenisimamia na kunivusha kwenye magumu mengi niliyopitia" alisema Zumaridi.

Alisema sherehe hiyo ya kihistoria itaambatana na keki iliyobeba ujumbe wa maisha yake.

Pia Mfalume Zumaridi alitumia fursa hiyo kuwaombea waandishi wa habari ili wazidi kufanya kazi kwa weledi na kuwaelusha na changamoto pamoja kuombea amani na utulivu wa Taifa ambayo ni tunu iliyowekwa na Mwenyezi Mungu.
Na Hellen Mteleko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.