LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wachimbaji madini watakiwa kujiandaa na zoezi la kusajiliwa kidijitali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wachimbaji madini nchini wametakiwa kujiandaa na kushiriki ipasavyo zoezi la uandikishaji vitambulisho vya kidijitali ambavyo vitawasaidia kutambulika na kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za kibenki.

Rai hiyo imetolewa Juni 28, 2023 na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina wakati akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa vitambulisho vya kidijitali kwa wachimbaji madini nchini iliyofanyika jijini Mwanza.

Bina amesema vitambulisho hivyo vya kidijitali vitasaidia kuwatambua wachimbaji madini nchini na pia kuleta manufaa kupitia FEMATA hivyo ameshauri kila mmoja aliye kwenye mnyororo wa sekta ya madini kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika nchi nzima.

"Kitambulisho knakusaidia kutambulika na kuepuka usumbufu usumbufu ambao umekuwa ukiwakumba wachimbaji hususani wakati wanasafirisha madini wakihisiwa ni wezi wa madini" amesema Makamu wa Rais FEMATA, Alfred Luvanda.

Naye Mhazini Mkuu FEMATA, Gregory Kibusi ametaka manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na kuwatambua wachimbaji madini kupitia kanzi data yao, utambulisho wa wachimbaji wakati wa majanga kama ajali migodini, kuwatambulisha katika huduma za kifedha na bima za afya.

Amesema gharama za kitambulisho hicho ni shilingi za kitanzania Tsh. 30,000 ambapo kati ya hizo, mtoa huduma atachukua Tsh. 18,720 na FEMATA Tsh. 11,280 ambazo itagawana na REMA (REMA asilimia 60 na FEMATA asilimia 40).

"Ni mradi mkubwa hivyo tuupokee kwani utatusaidia pia kupata mapato yatakayotusaidia kujiendesha ambapo fedha itakayopatikana itagawanywa kwa FEMATA na Vyama vya Wachimbaji Madini vya Mikoa. Tunaomba Serikali kupitia Ofisi za Maafisa Madini Wakati wa Mikoa itusaidie kupata taarifa za wamiliki wa leseni ili iwe rahisi kuwafikia wachimbaji madini" amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi FEMATA, Tariq James.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Afisa Madini Mkazi Mkoa Mwanza, Mhandisi Ndembi Tuma ameshauri FEMATA kutoa elimu ya kutosha kwa wachimbaji madini nchini ili kushiriki zoezi hilo la usajili wa vitambulisho vya kidijitali huku akisema Serikali iko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi hilo na kuwafikia wachimbaji wote kuanzia wenye leseni, mialo na maduara.

Zoezi la usajili wa wachimbaji madini nchini linatarajiwa kuanza hivi karibuni ikiwa ni ushirikiano baina ya FEMATA na kampuni ya TNT Resources ya nchini Uholanzi hivyo wadau wote walio kwenye mnyororo wa sekta ya madini wamehimizwa kutoa ushiriano wa kutosha ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha kuhusu mradi wa vitambulisho vya kidijitali kwa wachimbaji madini nchini iliyofanyika Juni 28, 2023 jijini Mwanza na kuwashirikisha viongozi wa Vyama vya Wachimbaji Madini wa Mikoa.
Washiriki wakifuatilia warsha kuhusu mradi wa vitambulisho vya kidijitali kwa wachimbaji madini nchini iliyofanyika jijini Mwanza.
Makamu wa Rais FEMATA, Alfred Luvanda akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo.
Mhazini Mkuu FEMATA, Gregory Kibusi akielezea manufaa ya zoezi la utoaji vitambulisho kwa wachimbaji madini nchini.
Mradi wa vitambulisho vya kidijitali kwa wachimbaji madini unatarajiwa kuleta tija mbalimbali ikiwemo kuwa na kanzi data itakayowezesha wachimbaji kutambulika na kunufaika na huduma muhimu ikiwemo za kifedha/ kibenki.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa Mwanza, Malale Lutoja akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mwakilishi wa Afisa Madini Mkazi Mkoa Mwanza (MWAREMA), Mhandisi Ndembi Tuma akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa Mara (MWAREMA), David Bita akichangia hoja kwenye warsha hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano FEMATA, Dkt. Benard Joseph akizungumza kwenye warsha hiyo.
Afisa Miradi kampuni ya TNT Resources ya nchini Uholanzi, Sharon Sheffet iliyoingia ubia na FEMATA kwa ajili ya kuendesha zoezi la kuandikisha wachimbaji madini nchini akizungumza kwenye warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye warsha hiyo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.