LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la WOTESAWA lawatunuku vyeti Wanahabari Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani WOTESAWA limewatunuku vyeti vya pongezi waandishi wa habari saba kutoka vyombo mbalimbali vya Habari akiwemo George Binagi kutoka BMG Online na Alloyce Nyanda kutoka Star TV.

Waandishi wa habari wengine waliotunukiwa vyeti hivyo ni Moses Methew- TBC, Sada Amir- Mwananchi, Judith Ferdinand- Majira, Michael Gabon- Kwizera FM na Sharifa Suleiman- RFA.

Waandishi hayo wamekabidhiwa vyeti hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani yaliyofanyika Juni 16, 2023 jijini Mwanza yakiambatana na Siku ya Mtoto wa Afrika.

Msimamizi wa Makao na Uwezeshaji kutoka shirika la WOTESAWA, Demitila Faustine amesema hatua hiyo ni sehemu ya kutoa hamasa kwa waandidhi wa habari ili kuendelea kufanya kazi kuitetea jamii wakiwemo wafanyakazi wa nyumbani.

Alisema waandishi wa habari wana mchango mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii hivyo shirika la WOTESAWA limetambua mchango wao na kuwakabidhi vyeti hivyo na kuwahimiza kuendelea kuandika habari kuhusu stahiki za wafanyakazi wa nyumbani.

“Tunashukuru WOTESAWA kwa kutambua mchango wetu, vyeti hivi vitakuwa chachu kwetu na kwa wengine kuongeza hamasa ya kufanya kazi kwa bidhii hususani kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani” alisema Alloye Nyanda kutoka Star TV.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti George Binagi kutoka mtandao wa BMG.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Judith Ferdnand kutoka Gazeti la Majira.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Sada Amir kutoka Gazeti la Mwananchi.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Sharifa Suleiman kutoka RFA.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Alloyce Nyanda kutoka Star TV.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Michael Gabon kutoka Kwizera FM.
Afisa Kazi Mkoa Mwanza, Betty Mtega (kushoto) akimkabidhi cheti Moses Methew kutoka TBC.

No comments:

Powered by Blogger.