LIVE STREAM ADS

Header Ads

Yaliyojiri kwenye Kilele cha Siku ya Mabaharia Duniani 2023 kitaifa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla akiwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani iliyoadhimishwa kitaifa jijini Mwanza Juni 25, 2023 katika uwanja wa Furahisha.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 22- 25, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Huduma za Meli na Bandari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA), Rajab Ally Rajab akizungumza kwenye maadhimisho hayo na kuwataja mabaharia wawili waliotimiza vyema wajibu wao kazini na kuokoa maisha ya watu kwa ajili ili kukabidhiwa vyeti vya kuwatambua pamoja na zawadi.
Mkurugenzi wa Huduma za Meli na Bandari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA), Rajab Ally Rajab akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Meli na Bandari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA), Rajab Ally Rajab akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Meli na Bandari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA), Rajab Ally Rajab akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (kushoto) akimkabidhi cheti baharia Kapteni Josia Mwakibuja (kulia) ambaye alifanikiwa kuokoa zaidi ya abiria 2,000 kwa kutumia meli aliyokuwa akiiongoza katika eneo la Palma nchini Msumbiji wakati wa machafuko yaliyohusishwa na kundi la Alshabaab. Mwingine aliyekabidhiwa cheti kwenye maadhimisho hayo ni Baharia Amour Mussa Juma ambaye amehusika katika matukio zaidi ya 60 uokoaji baharini.
Picha ya pamoja.
Kapteni Josia Mwakibuja (kushoto waliosimama nyuma) na Baharia Amour Mussa Juma (kulia waliosimama nyuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali meza kuu.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Viongozi mbalimbali meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mshereheshaji Dotto Bulendu.
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mshereheshaji Dotto Bulendu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Maandalizi ya shughuli ya uokoaji majini.
Viongozi mbalimbali wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akikagua mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akikagua mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akikagua mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 22-25, 2023
Viongozi mbalimbali wa TASAC wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mabanda ya taasisi mbalimbali kwa ajili ya utoaji elimu kwa wananchi.
Watumiaji wa vyombo vya usafiri majini wakiwemo abiria wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira na kuepuka kutupa taka ovyo ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea ikiwemo kuathiri vyombo hivyo.

Rai hiyo ilitolewa Juni 25, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla kwenye kilele cha Siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Pia Masala alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na sekta ya ubaharia akisema idadi ya wanawake duniani bado iko chini ikilinganishwa na wanaume ambapo Shirika la Bahari Duniani linaweka wazi kwamba duniani kote kuna mabaharia milioni 1.6, Tanzania wakia takribani elfu tisa ambapo kati ya hao wanawake ni chini ya asilimia moja.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo, Stella Katondo alisema Tanzania imeridhia mkataba wa kimataifa wa kuzuia uchafunzi wa mazingira majini wa Marpol unaotaka vyombo vya usafiri majini na watumiaji wake kuhakikisha hakuna taka zinazoingia majini, kudhibiti umwagaji taka ikiwemo mafuta majini.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.