LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAMUFO yaomba elimu zaidi kwa wananchi kuhusu mkataba wa uwekezaji bandari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Stellah Joel.
Mlezi wa TAMUFO, Dk.Frank Richard. 

..............................................

Na Dotto Mwaibale, Arusha

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umeiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua faida ya mkataba wa bandari ya Dar es Salaam dhidi ya Kampuni ya DP World ya Dubai.

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana huku akielezea umuhimu wa uendelezaji wa bandari yetu ya Dar es Salaam kupitia mkataba huo.

“Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kuhusu uwekezaji wa uendeshaji wa bandari naona changamoto kubwa ni wananchi kutoa elewa vizuri juu ya uwekezaji huu ambao utaongeza pato la taifa,” alisema Joel.

Alisema watanzania siku zote ni waelewa na kuwa nchi yetu imekuwa na makampuni mengi ambayo yamewekeza katika maeneo mengi jambo ambalo ni la msingi katika kuinua uchumi.

Alisema tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha ridhia mkataba huo baada ya kujiridhisha kuwa utakuwa na tija hivyo kazi kubwa iliyopo ni kwa wanasheria na wataalamu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutoka na kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida ambayo nchi itaipata kupitia uwekezaji huo.

Mlezi wa TAMFO, Dk.Frank Richard alisema Serikali iliridhia mkataba huo baada ya kupitia mawasilisho ya kampuni hiyo pamoja na sifa zao kimataifa na kuamua kuanzisha majadiliano na kampuni ya DP World kwa kuzingatia uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini.

Alisema suala hili lisitugawe watanzania kwa namna moja ama nyingine kwani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hawezi kuiuza bandari ambayo ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi kwani ana lengo zuri la kuongeza mapato kupitia uwekezaji huo mkubwa wenye tija.

Alisema kupatikana kwa mapato mengi katika nchi kunatoa fursa na kwa wanamuziki kupata fedha kutokana na kuimalika kwa uchumi na mzunguko wa fedha kuwa mkubwa.


No comments:

Powered by Blogger.