LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023 Buchosa wilayani Sengerema

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge wa Uhuru umewasili katika Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambapo utakimbizwa umbali wa kilomita 143 ukikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1.

Mwenge huo umewasili katika Halmashauri ya Buchosa, Jumapili Julai 16, 2023 ukitokea wilayani Nyamagana ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Amina Makilagi ameukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga kwa ajili ya kukimbizwa kwenye Wilaya yake yenye Halmashauri mbili ambazo ni Buchosa na Sengerema.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuhitimisha mbio zake mkoani Mwanza Julai 21, 2023 na kuelekea mkoani Simiyu ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai, Kwa Uchumi wa Taifa".
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Tazama picha zaidi kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Buchosa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Iseni.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akimlaki Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2023, Abdalla Shaib Kaim (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (wa pili kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (wa pili kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (wa pili kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (wa pili kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (kushoto) baada ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru.
Viongozi mbalimbali wakipokea Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo akitoa salamu wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ambapo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa barabara ya lami kuelekea Nyehunge na hivyo kuondoa atha waliyokuwa wanakabiliana nayo wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.