LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Sima awahimiza wananchi kumuombea Rais Samia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mbungewa Singida Mjini Musa Sima, akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Unyianga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero aliyoifanya Julai 18, 2023.
..................................................................



Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida mjini, Musa Sima amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa mno na amewaomba watanzania kumuombea ili Mungu aendelee kumpa afya njema na maisha marefu yenye baraka na fanaka katika kuliongoza Taifa letu.

Sima ameyasema hayo Julai 18, 2023 wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Unyianga iliyopo Manispaa ya Singida katika mkutano wa hadhara alioufanya baada ya kutembelea miradi ya maendeleo na kuikagua katika muendelezo wa ziara yake alioianza juzi jimboni humo.

Alisema Rais Samia amekuwa akifanya kazi kubwa na ngumu yenye uadilifu hivyo kila mpenda maendeleo hapa nchini anapaswa kumpongeza na kumuombea.

"Mimi na wenzangu wa maeneo mengine ambao tumenufaika na uongozi wake katika awamu yake hii ya sita tunakilasababu ya kumtolea salamu za kumshukuru mbele yenu yeye hawezi kufika hapa na tulipokuwa tunazungumzia mafiga matatu tunaanza na la kwake, mbunge na diwani," alisema Sima.

Alisema kazi katika nchi hii imefanyika kubwa na kuwa Rais Samia sio msemaji sana kama walivyo wanawake wengine wao ni watendaji wakuu na watu wenye huruma kwani wakisema bungeni anawasikiliza na wanapoizungumzia Singida imepata miradi mikubwa na yenye fedha nyingi sana.

"Ndugu zangu tumepata miradi ya maji, umeme, barabara, afya na kila kitu, nilipokuja mara ya kwanza hapa changamoto kubwa ilikuwa ni maji na sio hapa tu bali ilikuwa karibu maeneo mbalimbali ya jimbo la Singida mjini na hela tuliyokuwa tukiipata ilikuwa ndogo bilioni 2 au 3 na kuigawanya kwenye maeneo yote ilikuwa ni changamoto lakini umetokea mradi wa maji wa miji 28 kwa nchi nzima na moja ya miji hiyo ilionufaika ni Manispaa ya Singida ambapo tupewa Sh.Bilioni 40 jambo ambalo litaweza kurudi bungeni na kuomba fedha za maji nitachekwa," alisema Sima huku akishangiliwa na wananchi.

Alisema kupitia mradi huo wananchi wajue wanakwenda kusahau kabisa kama walikuwa na changamoto ya maji ndani ya Manispaa ya Singida kwani watayatumia na kubaki na ziada kubwa hivyo wamshuruku Rais Samia kwa kutoa fedha hizo ambazo tayari zipo kwa wataalam na kazi hiyo ya ujenzi imeanza ambapo hadi kukamilika itachukua miezi 12 hadi 24 kwa jimbo zima na akawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wa mradi huo pamoja na kuitunza miundombinu.

Sima alisema yeye tangu awe mbunge fedha alizopata kwa ajili ya kutekeleza miradi katika jimbo lake ni nyingi mno achilia mbali majimbo mengine nchini kote sasa inakuwaje watu wasema hakuna kazi iliyofanyika chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Sima akizungumzia kazi nyingine kubwa aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan ni kupokea maombi yake ya kuomba majengo ya iliyokuwa Hospitali ya Mkoa wa Singida yatumike kuwa Hospitali ya Wilaya (Hospitali ya Manispaa Singida) ili wananchi waendelee kupata huduma karibu na gharama zake zitakuwa nafuu kwa wale ambao watakuwa hawana bima.

Alisema kama haitoshi wamejenga vituo vya afya viwili, Unyambwa, Mwaja na bado kwa kupitia mapato ya ndani wameshirikiana na madiwani wamejenga kituo cha afya Kata ya Mtipa na sasa wanakamilisha Zahanati katika Kata hiyo ya Unyianga ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na Serikali ikawapa sapoti.

Mbunge Sima akiendelea kuzungumzia uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam alisema haijauzwa isipokuwa wananchi wanachanganywa kutokana na jambo hilo kuwa na maneno mengi kutoka kila pande.

Alisema wananchi wanapaswa kuwauliza wabunge kile walichokiridhia na kukipitisha badala ya kuyumbishwa na maneno ya watu ambayo hayana tija katika uwekezaji huo mkubwa wenye manufaa kwa Taifa.

Alisema katika nchi hii uwekezaji haujaanza leo na fedha nyingi za miradi inayotekelezwa zinatokana na uwekezaji na ndani ya Manispaa ya Singida akianza kujumulisha miradi ya elimu, afya na barabara hazipungui bilioni 10 akichanganya na bilioni 41 za mradi wa maji, Tanroads, Tarura, umeme zinaweza kukaribia kufika hadi Sh. Trilioni moja katika kipindi cha muda mfupi alichokaa madarakani Rais Samia Suluhu Hassan.

"Kwanini nisitumie fursa yangu kumuombea mama huyu kwa Mungu ili aendelee kuliongoza Taifa ili kwa maana tunapata fedha nyingi sana," alihoji Mbunge Sima huku akishangiliwa na wananchi.

Sima alisema fedha zote hizo zinakuja kutokana na uwekezaji hasa panapokuwepo na Rais mwenye maono ambaye anawajali wananchi wake kwa kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana.

Alisema leo anakuja mwekezaji lakini wakati huohuo kuna watu wanaibuka kufanya upotoshaji ili kukwamisha uwekezaji huo watu hao hawaitakii mema nchi yetu na wana lengo la kuwagawa watanzania.

Alisema wabunge wanaowajibu wa kuridhia makubaliano ya mkataba kati ya Tanzania na nchi nyingine kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 tatu.

Alisema wakiwa wawakilishi wa wananchi walichokiridhia ni sahihi hakuna eneo waliloridhia kwa ajili ya kuliangamiza taifa la Tanzania.

Awali kabla ya Mbunge Sima hajazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara Diwani wa Kata hiyo, Geofrey Mdama alipata fursa ya kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi ambapo naye alitumia nafasi hiyo kumpongeza.

Mbunge Sima akiwa akiwa katika ziara hiyo aliongozana na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Singida ambapo alitembelea Shule ya Sekondari ya Unyianga na kuzungumza na wanafunzi pamoja na walimu kabla ya kweda kukagua ujenzi wa Zahanati ya Unyianga.

Katika ziara hizo za Mbunge Sima wananchi wamekuwa wakionesha imani kwake kutokana na jinsi ambavyo anawatumikia na kufikia hatua ya kushindwa kuvumilia na kuonesha upendo wao wa dhahiri kwake huku wakimshukuru kwa ushirikiano anaowapa na kujitoa kuwasadia katika shughuli mbalimbali ambapo amekuwa akizawadiwa zawadi na kufanyiwa dua.

Katika mkutano huo wananchi walimpa zawadi ya kuku na mbuzi pamoja na diwani wa kata hiyo Geofrey Mdama ambapo pia wanawake 10 kutoka vyama vingine wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata hiyo Elizabeth Benedict ambao wamejiunga na CCM kufuatia kuridhishwa na kazi nzuri za maendeleo zinazofanywa na Rais Samia,Mbunge wao Musa Sima na Diwani Geofrey Mdama.



Kesho Mbunge Sima anatarajia kuendelea za ziara yake kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Kisaki na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara akiongozwa na diwani wa kata hiyo, Moses Ikaku.



Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama, akizungumza kwenye mkutano huo.V
Vijana wa bodaboda wakiongoza msafara wa Mbunge Sima wakati wa kwenda kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima, akiwasalimia Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Unyianga wakati wa ziara hiyo.
Mbunge Musa Sima na viongozi wengine wakiwasalimia kwa kuwapungia mikono Wanafunzi wa Sekondari ya Unyianga.


Muonekano wa Zahanati ya Kata ya Unyianga ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Unyianga, Ally Hassan (kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Unyianga.
Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama, akitoa maelekezo mbele ya Mbunge Sima, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo.
Muonekano wa Zahanati hiyo kwa sasa.
Mbunge Sima akisalimiana na wanawake wa kata hiyo.
Wanawake wa Kata ya Unyianga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wazee wa kata hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Unyianga, Charles Mtaturu, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyianga A, Issa Ramadhan na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyianga B, Gidion Kisuke.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
Mzee Shadrack Siju akiongoza maombi wakati wa kufungua mkutano huo.
Sheikh wa Kata ya Unyianga, Hamisi Mkanga, akiomba dua kabla ya kuanza mkutano huo.
Wataalam wa Kata ya Unyianga wakijitambulisha.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyianga B, Gidioni Kisuke, akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi waliwa meza kuu.
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Unyianga, Lue Milado, akiongoza mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo.
Katibu wa CCM wa kata hiyo, Joseph Martin akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Seif Nyangu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyianga A, Issa Maliwa, akifungua mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Singida, Ramadhan Mtipa, akizungumza wakati akitambulisha wajumbe wenzake kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa kamati ya siasa wa Wilaya ya Singida, Hawa Ntandu akijitambulisha.
Mbunge Sima, akicheza sanjari na wakina mama wakati wa mkutano huo.




Mkazi wa Kata ya Unyianga, Shabani Kasenya na Mbunge Sima wakionesha umahiri wa kucheza ngoma ya asili ya kabila la kinyaturu wakati wa mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama, akizungumza kwa upendo na wakina mama kabla ya kuanza kuzungumza kwenye mkutano huo.
Wakina Mama wakionesha upendo wa kumkumbatia mbunge wao Musa Sima kabla ya kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge Musa Sima akimtambulisha rasmi Diwani ya Kata hiyo Geofrey Mdama kuwa ni Makamu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, baada ya kuchaguliwa hivi karibuni kushika nafasi hiyo.
Mhandisi wa Maji kutoka SUWASA, akielezea kuhusu mradi wa maji wa miji 28 ambao mji wa Manispaa ya Singida nao wameupata.
Mbunge wa Singida mjini, Musa Sima akiwa amejitwika kibuyu cha asili cha kimila cha kabila la wanyaturu alichopewa na wanawake wa kata hiyo ikiwa ni heshima kwake na kuenzi mchango wake mkubwa wa kuwatumikia katika kuwaletea maendeleo. Katika tukio hilo alipewa na kuku jogoo.
Mbunge Sima akiwa na mbuzi aliyepewa na wazee wa kata hiyo ikiwa ni kumshukuru kutokana na mchango wake wa kuwaletea maendeleo.
Baadhi ya wanawake wa kata hiyo wakiwa wamejipanga foleni wakisubiri kupewa kadi baada ya kujiunga na CCM wakitokea vyama vingine vya siasa baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayofanywa na Rais Samia, Mbunge wao Musa Sima na Diwani wa kata hiyo, Geofrey Mdama..
Wanachama 10 wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kadi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima akiwakabidhi mpira wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Unyianga.

No comments:

Powered by Blogger.