LIVE STREAM ADS

Header Ads

Misungwi waomba Waziri kuingilia kati utekelezaji wa miradi ya maji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza limeeleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri hiyo na kuomba Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuingilia kati ili ikamilike na kutoa huduma kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kashinje Erasto ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2022/23 kilichoketi kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za miradi ya maendeleo.

Amesema bado kuna utekelezaji wa kusuasua katika miradi ya maji ikiwemo mradi wa Idetemya, Lujamate- Buhingo, Mbalika- Misasi, Bulemeji- Ukirigulu na Usagara- Sumve ambayo kwa pamoja inagharimu zaidi ya bilioni 90.

"Waziri aje Misungwi aone miradi ya maji inavyotekelezwa chini ya kiwango na bila kukamilika kwa wakati huku wananchi wakiendelea kutaabika na maji. Tuna chanzo cha maji Ihelele kinachopeleka maji Kahama, Tabora hadi Dodoma lakini wananchi wa pale hawana maji, Serikali iangalie namna ya wao pia kupata maji" amesema Kashinje.

Katika kikao hicho taarifa iliyowasilishwa na RUWASA ilieleza kuwa hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri ya Misungwi ni zaidi ya asilimia 90 ambapo hata hivyo madiwani waliikataa taarifa hiyo wakisema adha ya upatikanaji wa maji ni kubwa kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kashinje amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ilifanikiwa kufikia lengo la kukusanya mapato kiasi cha shilingi bilioni 3.1 na kwa mwaka 2023/24 imelenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 4.8.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Kashinje Erasto (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Kashinje Erasto (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo. 
Waliokaa kutoka kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza (Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi), Afisa Tawala Misungwi, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Rahma Fidelis (kushoto) akiwashukuru madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuendelea na nafasi hiyo kwa awamu nyingine ya mwaka wa fedha 2023/24.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Rahma Fidelis (kushoto) akiwashukuru madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuendelea na nafasi hiyo kwa awamu nyingine ya mwaka wa fedha 2023/24. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kashinje Erasto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Kijamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi akiwashukuru madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kuidhinisha wenyeviti wa Kamati zote pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuendelea kushika nafasi zao kwa awamu nyingine ya mwaka wa fedha 2023/24.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza (Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi), Kusirie Swai akitoa maelekezo ya Serikali wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambayo ni pamoja na kusimamia vyema miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na miradi hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza (Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi), Kusirie Swai akitoa maelekezo ya Serikali wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa kwenye kikao cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/23 ambapo pamoja na mambo mengine walieleza kutoridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji.
Watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichojadili taarifa mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa robo ya nne ya mwaka bajeti 2022/24.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.