LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wakabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole 'Biometric Fingerprint' katika mikoa ya Mara na Simiyu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Mratibu wa PEPFAR Tanzania, Jessica Greene akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi (kulia) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa (kushoto).
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kupitia Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kimetoa msaada wa vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) katika mkoa wa Mara na Simiyu kwa ajili ya utunzaji sahihi wa takwimu.

Vifaa hivyo vitasaidia kuondoa makosa na urudiaji wa usajili wa mteja pamoja na kutatua changamoto ya utambuzi wa kawaida wa wateja wapya na wa zamani wanaopata huduma katika vituo vya tiba na matunzo.

Hafla makabidhiano ya vifaa hivyo imehudhuriwa na Mratibu wa PEPFAR Tanzania, Jessica Greene, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dk. Mahesh Swaminathan, Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania
Dkt. George Mgomella, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu ikiganyika Agosti 15, 2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi.

Mkurugezi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaotekelezwa na Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC)

“Kwa muongozo wa Wizara ya Afya (NACP), Amref Tanzania imenunua vifaa vya utambuzi wa vidole ( Biometric fingerprint) 155 vyenye thamani ya shilingi Milioni 25 kwa mkoa wa Mara ikiwa ni sehemu ya vifaa vya utambuzi 398 tulivyotoa kwa ajili ya Mikoa mitatu ya Tanga (vifaa vya utambuzi 108) na Simiyu (vifaa vya utambuzi 135) ambapo vifaa vyote vya utambuzi 398 vina thamani ya dola za Marekani 20,000.7"

Pia tumetoa mafunzo kwa vitendo kwa viongozi wa Afya wa Mkoa na wilaya na wahudumu wa Afya kwa halmashauri zote juu ya matumizi ya utambuzi wa vidole kupitia mfadhili PEPFAR” ameongeza Dkt. Florence.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu.

“Hadi sasa hapa mkoani Mara tangu tuanzishe huduma hii ya kutumia vifaa vya utambuzi wa vidole kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanaopata huduma katika vituo vya tiba na matunzo tumeweza kusajili wateja takribani 3000 kwa utambuzi wa vidole kati ya wateja 63,000 (6%) walio kwenye dawa . Kwa kipindi cha wiki mbili na wateja wote wanaendela na kutumia mfumo huu wa kisasa wa utambuzi wa vidole. Kwa mantiki hii, kupitia vifaa hivi vya kisasa kuna ufanisi mkubwa katika utambuzi wa wateja, utunzaji sahihi wa takwimu za wateja wa VVU katika kitengo cha Utunzaji na Matibabu ya Virusi Vya Ukimwi (Care and Treatment centre)” ameongeza Dkt. Frolence.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi, ameipongeza Serikali ya Tanzania na mfadhili PEPFAR kupitia CDC Tanzania na mdau Amref Health Africa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya afya kupitia miradi mbalimbali ya afya hapa nchini.

“Hivi karibuni tu PEPFAR ilikuwa inaadhimisha Miaka 20 ya uwepo na utekelezaji wa mfuko huko tangu kuanzishwa kwake na Tanzania ikiwa moja wa nchi inayonufaika na mfuko huo. Binafsi nawapongeza sana Kwa kujali maendeleo ya sekta ya afya kwa Manufaa ya wanajamii wote. Chini ya Ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC Tanzania, Amref Tanzania imekuwa ikitekelza huduma za afya mkoani Mara” amesema .
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi.

Lusasi ameishukuru Amref Health Africa Tanzania kuendelea kuboresha mifumo ya takwimu na taarifa katika vituo vinavyopewa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC mfano Chini ya ufadhili wa PEPFAR, kupitia CDC Mradi umekuwa ukitoa msaada katika mkoa huo kama utunzaji wa takwimu (Data Management), Uchambuzi wa takwimu (Analysis,) na Utoaji wa Taarifa sahihi ( Reporting).

“Misaada mingine wanayotoa ni kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa takwimu kupitia mafunzo ya darasani na vitendo katika maeneo ya kazi. (on Job training and Mentorship), Mradi unatoa usimamizi wa kuunga mkono (Supportive supervision) katika shughuli za tathmini na ufuatiliaji (M&E) ili kuboresha ubora wa takwimu. Pia Mradi unatoa mafunzo ya kazini (on Job training) kwa watumishi wa takwimu na watumishi wengine wa afya katika vituo vyetu na Mradi huu umetoa ajira kwa Data Clerks wapatao 110 kwa mkoa wa Mara” amesema Kisasi.

Lusasi ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa afya na watu wote watakaotumia vifaa hivyo wawe waaminifu na waadilifu wahakikishe wanavitunza na yeyote atakayeleta uzembe na kusababisha uharibifu au upotevu hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi (kulia) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa (kushoto)

Naye Mratibu wa PEPFAR Tanzania, Jessica Greene amesema Amref Tanzania inatoa huduma jumuishi za kina katika vituo na jamii kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR ili kuunga mkono malengo ya kimataifa juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yaani UNAIDS 95-95-95 na imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na uongozi wa afya ngazi ya mkoa katika kuboresha shughuli za Tathmini na Ufatiliaji (M&E).

Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan amesema matumizi ya Biometric Fingerprint yatasaidia sana kukabiliana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma na kwamba ili kuhakikisha mfumo huo unafanikiwa watumishi wa afya wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo vizuri.
Maboksi yenye vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint)

Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania, Dkt. George Mgomella amesema matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole yatasaidia sana kuongeza usiri kwa wateja kwani sasa hawatatembea na kadi za utambuzi na wataweza kutumia huduma popote, na itarahisisha kujua idadi halisi ya wateja na kuondoa changamoto ya kwamba wateja wanapotea katika huduma endapo wataondoka kwenye kituo kimoja kwenda kituo kingine.

Amesema mfumo huo wa kisasa unalenga kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa katika vituo vya afya ili kuweza kusaidia katika kufanya maamuzi kwa hatua ya kituo hadi mkoani (Improved data ownership) Chini ya Ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC Tanzania.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Zabron Masatu na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole ( Biometric Fingerprint) wameishukuru Amref Tanzania kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa takwimu sahihi kwa ajili ya matokeo sahihi ili kuboresha huduma za afya.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi Jumanne Agosti 15, 2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dominicus Lusasi (kulia).
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Viongozi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kutoka kwa Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu.
Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu akionesha namna vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) vinavyofanya kazi.
Viongozi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kutoka kwa Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) Tanzania Dkt. Mahesh Swaminathan akielezea kuhusu vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint).
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu akielezea kuhusu vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint).
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya Mkoa wa Mara na Simiyu.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya Mkoa wa Mara na Simiyu.
Mratibu wa PEPFAR Tanzania, Jessica Greene akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya mikoa ya Mara na Simiyu.
Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania,
Dkt. George Mgomella akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya mikoa ya Mara na Simiyu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniphace Marwa akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya mikoa ya Mara na Simiyu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Zabron Masatu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric Fingerprint) kwa ajili ya mikoa ya Mara na Simiyu.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania Dkt. Florence Temu (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dkt. Mahesh Swaminathan (katikati) na Mratibu wa PEPFAR Tanzania, Jessica Greene (kulia) wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu.

No comments:

Powered by Blogger.