LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM yazindua kampeni za uchaguzi mdogo Mwaniko, Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mwaniko Wilaaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakimlaki mgombea udiwani wa Kata hiyo, Venance Mathias Ngwanza (aliyebebwa) wakati akiwasili kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika jumamosi Agosti 26, 2023. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023 baada ya aliyekuwa diwani wa Kata hiyo kufariki dunia.

Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Michael Lushinge Masanja 'Smart' amezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Mwaniko wilayani humo na kutumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea wa chama hicho, Venance Mathias Ng'wanza.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jumamosi Agosti 26, 2023 katika Kijiji cha Mwaniko, Smart amesema CCM imemsimamisha mgombea udiwani mwenye uwezo mkubwa wa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na Serikali kuwaletea maendeleo.

"Kwa mambo haya makubwa anayoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo ujenzi wa shule mpya, barabara na maboresho katika Kituo cha Afya, atawashangaa tukimchagua mgombea wa chama cha upinzaji" amesema Smart akimnadi mgombea huyo wa CCM Kata ya Mwaniko ambapo uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023 baada ya aliyekuwa diwani wa Kata hiyo kufariki.

Smart amesema mgombea huyo ana uwezo mkubwa wa kujisimamia na kujiongoza hivyo hiyo ni ishara kwamba pia ana uwezo wa kuwaongoza wengine kwa weledi kwani ni kijana msomi. "Rais ni wa CCM na mbunge wa CCM, msikosee mkatuwekea guzi katikati, tochi haitawaka" amesema Smart akimuombea kura mgombea huyo.

Naye mgombea udiwani huyo, Venance Mathias Ng'wanza amesema akifanikiwa kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Mwaniko atashirikiana vyema na viongozi wa chama na Serikali ili kuhakikisha Kata hiyo inasonga mbele zaidi kimaendeleo.

"Wana Mwaniko mmepata mwamba kweli kweli, yajayo yanafurahisha, natamani Kata yetu iwe kama mji Sayuni. Naomba kura zenu tarehe 19, 2023 maana CCM imeniamini, Kata yetu inaenda kutikisa kwa maendeleo" amesema Ng'wanza.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Michael Lushinge Masanja 'Smart' (kushoto) akimtambulisha mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani humo, Venance Mathias Ng'wanza (kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo ulioanyika Jumamosi Agosti 26, 2023 katika Kijiji cha Mwaniko ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Michael Lushinge Masanja 'Smart' (kushoto) akimkaidhi Ilani ya Uchauzi mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani humo, Venance Mathias Ng'wanza (kulia). Uchaguzi katika Kata hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023 baada ya aliyekuwa diwani wake kufariki dunia.
Mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilaya Misungwi, Venance Mathias Ng'wanza (kulia) akiomba kura kwa wananchi wa Kata ya Mwaniko. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Michael Lushinge Masanja 'Smart'.
Mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi kupitia CCM, Venance Mathias Ng'wanza (katikati) akifurahia mapokezi ya wananchi na makada wa CCM Kata ya Mwaniko wakati wa ufunguzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023.
Mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi kupitia CCM, Venance Mathias Ng'wanza (katikati) akifurahia mapokezi ya wananchi na makada wa CCM Kata ya Mwaniko wakati wa ufunguzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023.
Mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi kupitia CCM, Venance Mathias Ng'wanza (katikati) akifurahia mapokezi ya wananchi na makada wa CCM Kata ya Mwaniko wakati wa ufunguzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Septemba 19, 2023.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Michael Lushinge Masanja 'Smart' (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Mwaniko.
Mgombea udiwani Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi kupitia CCM, Venance Mathias Ng'wanza (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM.
Viongozi wa CCM wakifuatilia ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi.
Kada wa CCM Kata ya Mwaniko akiwa na picha ya mgombea udiwani katika Kata hiyo, Venance Mathias Ng'wanza.

No comments:

Powered by Blogger.