LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mradi wa Vanilla waanzishwa nchini Kenya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya (kushoto) akipiga picha na wadau
****

Kampuni ya Vanilla International Limited imeanzisha mradi wa VANILLA VILLAGE KENYA, Mombasa nchini Kenya katika mji mdogo wa Mariakani.

Mkurugenzi wa Vanilla International Limited Duniani Simon Mnkondya amechukua uamuzi huo baada ya kuona Wakenya wengi wanachangamkia katika kilimo cha Vanilla kuliko hata watanzania licha ya kwamba tumekuwa tukifanyia mradi wa VANILLA ARUSHA,ZANZIBAR na VANILLA VILLAGE DODOMA.

Mnkondya amesema ni wakati sahihi kwa Kenya kuanza kilimo cha VANILLA kwa mfumo wa mashamba Shufwaa yaani Block Farming ili kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha Uwepo wa Soko la Vanilla.

WASHIRIKA
Vanilla International Limited itafanya mradi ikishirikiana Na Taasisi ya MRM Foundation na Karibuni Foundation zote za Kenya na Taasisi ya Society Watch ya Tanzania.

Lengo la mradi wa VANILLA VILLAGE KENYA ni kukuza uchumi wa Wakenya na Waafrika kwa ujumla kwa sababu bei ya vanilla imewahi kufikia mpaka Dola za Kimarekani 500$ takribani 1,000,000/= ya kitanzania.
Mkurugenzi wa Nyali Cinemax, Dipan Shah amesema Vanilla India imewafanya wakulima wawe matajiri sana kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani.

Naye Rais wa Upendo Foundation , bw. Bruno Cern'o mwenye Asili ya Italia amesema kwa vile vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa Waafrika kulima Vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.

Kwa upande wake Gianfranco Ranieri ambaye ni Rais wa KARIBUNI Foundation ya Milano Italia amesema atalima heka zaidi ya 100 hapa Kenya na anaenda kulima Vanilla kama Kichaa na atakuwa Kichaa wa Vanilla Kenya.

Naye Mama Siprosa Rabach Meneja mkazi wa MRM Foundation amesema lazima vanilla ilimwe Kenya watu wapate kazi na utajiri Kenya.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akizungumza na wadau wa kilimo cha Vanilla.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akizungumza na wadau wa kilimo cha Vanilla.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya.

No comments:

Powered by Blogger.