LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meya Sima akagua miradi ya elimu Mwanza, ampa heko Rais Samia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine amekagua miradi mbalimbali ya elimu ikiwemo ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Kanenwa iliyopo Kata ya Kishiri na kuelekeza ujenzi huo kukamilika mapema.

Sima amekagua Shule hiyo Agosti 11, 2023 na kutumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 540.3 kwa ajili ya mradi huo ambao itasaidia kuondoa adha kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda Shule.

Msimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Bukaga, Mwl. Mlingai Kasika amesema changamoto iliyopo ni ukosefu wa maji na hivyo kuomba Mstahiki Meya Sima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) kufikisha maji katika Shule hiyo kwani miundombinu yake ikiwemo vyoo inahitaji huduma hiyo.

Ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia 90 ukijumuisha vyumba 14 vya darasa la kwanza hadi darasa la saba, vyoo matundu 16, jengo la utawala na vyumba viwili vya madarasa ya awali.

Pia Mstahiki Meya Sima ameipongeza Kamati ya Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Ng'wang'halanga iliyopo Kata ya Buhongwa jijini Mwanza kwa kusimamia vyema fedha za mradi huo.

Sima baada ya kukagua mradi huo amesema Kamati hiyo imesimamia vyema fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kiasi cha shilingi milioni 540 ambapo mradi umefikia asilimia 96 ukitumia shilingi milioni 518 na kubakiza chenji zaidi ya shilingi milioni 22 ambazo zinaendelea kukamilisha hatua mbalimbali shuleni hapo.

Katika hatua nyingine Mstahiki Meya ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Nsumba na kushauri bweni hilo liitwe jina la Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kuenzi kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo anayoifanya.

Katika shule hiyo, shilingi milioni 240.5 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo, vyumba vinne vya madarasa na vyoo. Itakumbukwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilipokea zaidi ya shilingi bilioni moja kupitia mpango wa BOOST kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya elimu.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kulia) akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Msingi Kanenwa iliyopo Kata ya Kishiri jijini Mwanza.
Ujenzi wa Shule ya Msingi Kanenwa jijini Mwanza umefikia asilimia zaidi ya 90 na inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi ili kuondoa adha ya msongamano darasani.
Baadhi ya vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Msingi Kanenwa jijini Mwanza.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Msingi Kanenwa jijini Mwanza.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Msingi Kanenwa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine akiwa ameambatana na wataalamu wa halmashauri hiyo akikagua ujenzi wa shule ya msingi Kanenwa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) akikagua ujenzi wa shule ya msingi Kanenwa.
Watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara hiyo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine akikagua miradi ya elimu.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya msingi Ng'wang'halanga iliyopo Kata ya Buhongwa.
Ujenzi wa shule mpya ya msingi Ng'wang'halanga umefikia zaidi ya asilimia 96.
Mwonekano wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya msingi Ng'wang'halanga iliyopo Kata ya Buhongwa.
Mwonekano wa ndani, Shule mpya ya Msingi Ng'wang'halanga.
Shule mpya ya Msingi Ng'wang'halanga.
Mwonekano wa Shule mPya ya Msingi Ng'wang'halanga iliyopo Kata ya Buhongwa.
Mwonekano wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Nsumba iliyopo Kata ya Luchelele jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali.
Mwonekano wa bweni jipya katika Shule ya Sekondari Nsumba jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.