LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajawazito Kaliua mkoani Tabora waachana na imani potofu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wanawake wajawazito katika Kijiji cha Achawaseme Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wameanza kuhudhuria kliniki na kuachana na imani potofu iliyokuwepo hapo awali kwamba wakifanya hivyo watalogwa.

Katika Kijiji hicho baadhi ya wanawake walikuwa wakiaminikuwa ukiwa na ujauzito hupaswikwenda kliniki ama kuonekana hadharani kwani wabaya wako wanaweza kukufunga kishirikina naujauzito ukapotea ama ukachelewa kujifungua.

Mmoja wa wanawake katika Kijiji hicho, Khadija Mussa (40) mwenye watoto wawili amesema walikuwa na imani kwamba mwanamke akiwa na ujauzito anapaswa kwenda kwa mganga wa kienyeji ili akawekewe kinga ndipo ajifungue salama.

"Unakuta unaumwa kichwa, unaenda kwa mganga anakwambia umetegwa, anakuogesha madawa. Hali ikizidi kuwa mbaya ukienda hospitalini unaambiwa una malaria, sasa hapo unabaki unashangaa" amesema Khadija.

Hata hivyo Khadija amebainisha kuwa umbali wa kituo cha afya takribani kilomita 15 ulikuwa unasababisha wajawazito kutoenda kliniki hivyo aada ya Serikali kujenga Zahanati kijijini hapo mambo sasa yameanza kubadilika na wanawake wameanza kuwa na mwitikio wa kuhudhuria klini baada ya kupata elimu.

"Hospitali ilikuwa mbali, na pia tukaingiliwa sana na njia za kishirikina. Lakini hivi sasa Joyce (mhudumu wa afya ngazi ya jamii) ametutembelea na kutuelimisha hivyo wanawake wengi tunaenda kliniki" amesema Khadija.

Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Joyce Kinyega amesema baada ya Serikali kwa kushirikiana na mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAH kumjengea uwezo mwaka jana, tayari amewafikia wananchi zaidi ya 800 na kuwaelimisha kuhusu afya ya uzazi na umuhimu wa kuhudhuria kliniki.

Joyce amesema hapo awali imani potofu ikiwemo za kishirikina zilikuwa kikwazo kikubwa hususani kwa wanawake ambapo walikuwa tayari kwenda kwa waganga wa kienyeji kuliko kwenda klinikini.

"Walikuwa na mila na imani potofu kuhusu chanjo, walikuwa wakisema watoto wao watakuwa mazombi ama wakiwa wakubwa watakosa uzazi" amesema Joyce na kuongeza;

"Tunaishukuru Serikali ya mama Samia (Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan) kwa sasa hapa Achawaseme kuna Zahanati na tunaona mabadiliko makubwa kwani ndani ya mwezi huu akina mama 155 wamehudhuria kliniki na watoto wamepata chanjo" amesema Joyce akiongeza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wanawake kijijini hapo sasa wanahudhuria kliniki.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Joyce Kinyega akioa elimu ya afya ya uzazi kwa aadhi ya wanawake katika Kijiji cha Achawaseme Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.
Mwonekano wa Zahanati ya Kijiji cha Achawaseme Wilaya ya Kaliua mkoaniabora.

No comments:

Powered by Blogger.