LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi waipa kongole TANROADS Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi akiwa katika Mtambo wa kutengeneza Barabara.


Na Marco Maduhu - Kahama
Wananchi wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamepongeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ujenzi wa miundombinu imara ya Barabara, ambayo imekuwa kichocheo kikubwa cha uchumi,pamoja na akina mama wajawazito kuwahi kufika kwenye huduma za afya.

Wamebainisha hayo Septemba 04,2023 wakati wakizungumza na waandishi wa habari, walipofanya ziara kutembelea baadhi ya miundombinu ya Barabara ambayo imetekelezwa na TANROADS katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Miundombinu ya Barabara ambayo imetembelewa ni Mwabomba, Nonwe,Ulowa na Igombe Liver Barabara ambayo ni mpya inayounganisha Ushetu na Tabora yenye urefu wa Kilomita 25.

Baadhi ya wananchi ambao wametekelezewa miundombinu ya Barabara hizo akiwemo George Sengerema ambaye ni dereva wa magari, amesema awali barabara zilikuwa mbovu hazipitiki, na walikuwa wakiharibu vyombo vyao ya moto pamoja na kupata ajali za mara kwa mara.
Wananchi wakitumia Barabara ambazo ni imara zilizotengenezwa na TANROADS.

Amesema wanaishukuru Serikali kupitia TANROADS kwa kutengeneza barabara hizo ambazo zilikuwa korofi ambapo kwa sasa zipo imara na hakuna tena changamoto za ajali wala kuharibu magari yao.

"Barabara hizi awali zilikuwa mbaya sana hata kumpitisha Mjamzito ilikuwa Tabu mashimo kila mahali lakini sasa hivi tuna tereza tu kama tupo kwenye lami vile, tunaipongeza Serikali kwa ujenzi wa Barabara hizi" amesema Sengerema.

Naye Amosi Mataba mkazi wa Kaliua mkoani Tabora ameishukuru TANROADS kwa ujenzi wa barabara mpya ya Ushetu- Tabora ambayo kwa sasa bado ipo kwenye matengenezo akisema itawasaidia katika shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoani Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi amesema katika mwaka wa fedha (2022/2023) kwamba kilitengwa kiasi cha fedha Shilimgi bilioni 15 kwa ajili ya utengenezaji wa miundombinu ya Barabara mkoani humo.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi.


Amesema pia katika mwaka wa fedha (2023/2024) kimetengwa tena kiasi cha fedha Sh.bilioni 13.8 kwa ajili ya matengezo ya Barabara, na kubainisha katika barabara hiyo mpya ambayo inatoka Ushetu kuunganisha Tabora kwamba hadi kukamilika kwake pamoja na ujenzi wa daraja itagharimu bilioni 3.2.

Ametoa wito kwa wananchi kuitunza miundombinu hiyo ya Barabara, na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kando ya barabara, pamoja na madareva kuacha kupakia mizigo yenye uzito uliopitiliza na kuharibu barabara.
Mhandisi wa Idara Matengenezo, Midara Yaledi akizungumza kwenye ziara hiyo.
Msimamizi wa Mizani ya Mwendakulima wilayani Kishapu, Mhandisi Lugembe Vicent akizungumza kwenye ziara hiyo.
Dereva wa Bodaboda, Ngassa Samweli akipongeza utengenezwaji wa miundombinu ya Barabara.
Mwananchi Amos Mataba.
Magari yakipimwa uzito wa mizigo katika Mizani ya Mwendakulima wilayani Kahama.
Wananchi wakifurahia matengenezo ya miundombinu ya Barabara.
Ziara ikiendelea.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi akiwa katika Mtambo wa kutengeneza Barabara Mpya ambayo inaunganisha Ushetu na Tabora yenye urefu wa Kilomita 25.
Mitambo ikiendelea na matengenezo ya Barabara hiyo mpya.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi akiangalia moja ya Daraja ambalo wamelijenga katika kijiji cha Nonwe Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Mtambo ukiendelea na matengenezo ya Barabara mpya.
Mtambo ukiendelea na matengenezo ya Barabara mpya.
Mtambo ukiendelea na matengenezo ya Barabara hiyo mpya.
Waandishi wa Habari wakipiga picha ya Pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mibara Ndirimbi.

No comments:

Powered by Blogger.