LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Singida agiza udhibiti mianya ya upotevu wa mapato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba,l akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika baina yake na viongozi mbalimbali. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatma Mganga.


Na Dotto Mwaibale, Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha mashine za kukusanya fedha (POSS) zisitumike feki.

Serukamba ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri na wataalam mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika jana mjini hapa.

Amesema kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato na matumizi ya POSS feki hivyo kuukosesha mkoa kupata mapato stahiki ambapo aliviomba vyombo vya dola ikiwamo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kusaidia kufanya uchunguzi kwenye mageti ya ukaguzi wa mazao yanayosafirishwa.

Serukamba amesema Mkoa wa Singida unaweza ukawa kinara wa ukusanyaji wa mapato, uhifadhi wa mazingira na usimamizi wa miradi iwapo tu watendaji watafanya kazi kwa kujituma na kushirikiana badala ya kuyaachia baadhi ya makundi kufanya kazi hizo.

''Tukifanya kazi vizuri katika uhifadhi wa mazingira, ukusanyaji mapato, ukamilishaji wa miradi kwa wakati na kuwa timu moja, siku moja tutakuwa namba moja kitaifa'' amesema Serukamba.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizungumza kwenye kikao hicho amewaomba wakurugenzi pindi wanapopokea fedha za miradi kabla ya kuanza kutekelezwa watoke ofisini na kwenda kujua bei za vifaa badala ya kwaachia watu wa manunuzi pekee ambao wamekuwa na changamoto ya kuweka bei ya juu.

''Miradi mingi imekuwa haikamiliki kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali kumalizika kabla haijaisha na hiyo inasabishwa kununua vifaa kwa bei kubwa lakini wakurugenzi wakitoka na timu yao watawakuta wauzaji wa vifaa hivyo kwa bei ya chini'' amesema Mganga.

Mganga akitolea mfano amesema alipokuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wakati wanataka kutegeneza milango waliwaomba watu wa manunuzi wawape bei yao ambapo wasema ni Sh.Milioni 72 na walipotoka kutafuta bei kwa watu wengine alikuwepo wa Sh.Milioni 50 na mwingine Sh.Milioni 48 na hivyo kumpa kazi hiyo aliyekuwa na bei ya chini ambaye alifanya kazi hiyo kwa viwango vya hali ya juu.

Katika hatua nyingine Mganga amewaomba wakurugenzi hao kujenga tabia ya kwenda kujifunza kwa wenzao ambao wanafakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati na kwa fedha zilezile walizopokea kama wao.

Amesema utakuta Serikali imetoa fedha kiwango sawa lakini katika ukamilishaji wa miradi kwa fedha hizo hizo halmashauri zingine zinakamilisha miradi iwe ya ujenzi wa shule au vituo vya afya na halmashauri nyingine utakuta ujenzi wake upo hatua ya msingi.

Mganga amewahimiza watendaji hao kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla ya Agosti 9, 2023 ambapo ndio itakuwa kikomo cha fedha za bakaa na baada ya hapo zitarudi Serikalini.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine wakurugenzi na wakuu wa wilaya walitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato na miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye wilaya zao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akizungumza kwenye kikao hicho.
Wenyeviti wa Halmashauri wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, John Mgalula, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili akichangia jambo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula akiwa kwenye kikao hicho.

No comments:

Powered by Blogger.