LIVE STREAM ADS

Header Ads

Baraza la Wazee ACT Wazalendo launja ukimya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Baaza la wazee wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi limevunja ukimya na kuipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwekeza majengo ya ofisi na kitega uchumi kwa Mji wa Lindi.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Khalfani Zaidi ametoa pongezi hizo alipokuwa akisalimia wananchi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya kituo cha afya mjini Lindi.

Amesema kazi ya upinzani sio kulaumu Serikali iliyopo madarakani pale inapokosea bali ni pamoja na kupongeza inapofanya vizuri kwa wananchi inaowaongoza.

Amesema kitendo cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujenga ofisi ya idara ya uhamiaji na kitega uchumi ni cha kupongezwa na jamii inayopenda mandeleo ndio maana ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi wameamua kuipongeza wizara hiyo.

"Haya mawili yaliyofanywa na wizara kujenga majengo mawili ndani ya mji wetu, tunaipongeza kwa asilimia 40%" amesema Zaidi.

Pia ameutaka uongozi wa Wizara hiyo kuwakumbuka askari wake kuanzia jeshi la polisi, magereza, uhamiaji na zimamoto kwa kuwajengea nyumba za kuishi.

Zaidi amesema kazi inazofanywa na askari ni ngumu hivyo upo umuhimu na wao wakapatiwa nyumba nzuri za kuishi.

No comments:

Powered by Blogger.