LIVE STREAM ADS

Header Ads

Umoja wa wajasiriamali kwenye masoko na minada Mwanza (UWADOMAMI) watoa msaada Zahanati ya Nyakato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa wajasiriamali kwenye masoko na minada mkoani Mwanza (UWADOMAMI) umechangia ujenzi wa jengo la wagonjwa katika Zahanati ya Nyakato jijini Mwanza, kwa kukabidhi msaada wa nondo 15.

Zoezi la kukabidhi msaada huo limefanyika Jumatatu Novemba 06, 2023 likiongozwa na Mwenyekiti wa UWADOMAMI, Justine Sagara aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa umoja huo kwa niaba ya wananchama.

Sagara amesema hatua hiyo ni kutimiza ombi la diwani wa Kata ya Nyakato, Jonathan Mkumba alipohudhuria mkutano wa UWADOMAMI hivi karibuni ambapo aliomba wafanyabiashara kwenye masoko na minada kuchangia ujenzi wa jengo hilo.

"Jambo hili linaweza kuwa dogo lakini kwetu ni kubwa sana kwa sababu hatujawahi kuombwa msaada, ulikuja ukaomba na ukasikilizwa hivyo leo tuko mbele yako kukabidhi ndondo hizi ambazo zimenunuliwa kwa michango ya wadau wa minadani" amesema Sagara.

Sagara pia ametumia fursa hiyo kueleza kuwa UWADOMAMI iko tayari wakati wowote kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo msaada huo ni mwanzo tu wa kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano.

"Jengo hili likikamilika halitatoa huduma kwa wakazi wa Nyakato tu bali kwa watanzania wote wakiwemo wafanyabiashara wa minadani. Hata maeneo tunayofanyia shughuli zetu za minadani tumepewa na Serikali, lakini pia tumezungukwa na wananchi hivyo hatuna budi kuendelea kushirikiana" amesema Sagara.

Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba amesema jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kulaza wagozwa zaidi ya 40 na hivyo kusaidia Zahanati ya Nyakato kupanda hadhi kuwa Kituo cha Afya na kusogeza karibu huduma kwa wananchi na kukipunguzia mzigo Kituo cha Afya Buzuruga.

Mkumba amesema jengo hilo linahitaji nondo 60 kwa ajili ya kukamilisha ufungaji wa kufunga renta yote hivyo baada ya kupokea nondo 15 kutoka UWADOMAMI, bado kuna pungufu ya nondo 45 ambapo amewaomba wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo.

"Hadi kufika hapa ni nguvu za wananchi, tukimaliza kujenga boma Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan itamwaa fedha hapa kwa ajili ya kumalizia ujenzi huu na kuweka vifaa tiba ili wananchi waanze kupata huduma" amesema Mkumba huku akiwashukuru wale wote waliochangia ujengi huo.

Naye Afisa Mtendaji Kata ya Nyakato, Juma Ngoroma amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza mwezi Oktoba mwaka 2022 ambapo hadi sasa shilingi milioni 48 zimetumika na kwamba hadi kukamilika mwakani mwezi wa sita litagharimu shilingi milioni 210.

Kwa upande wake Mganga wa Zahanati ya Nyakato, Dkt. James Ishengoma amesema Zahanati hiyo ikipandishwa hadhi kuwa Kituo cha Afya itasaidia kuondoa adha kwa wananchi zaidi ya elfu 26 wa Kata ya Nyakato na hata wanaotoka nje ya Kata hiyo kwa kuongeza huduma mbalimbali ikiwemo kulazwa.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara (wa tatu kulia). 
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara.
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara.
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara.
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara.
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akipokea msaada wa nondo 15 kutoka kwa viongozi wa UWADOMAMI wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Justine Sagara (wa pili kulia).
Nondo 15 zilizotolewa na UWADOMAMI kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa katika Zahanati ya Nyakato jijini Mwanza.
Diwani wa Kata ya Nyakato, Jonadhan Mkumba (kushoto) akiwaonesha viongozi wa UWADOMAMI ulipofikia ujenzi wa jengo la wagonjwa katika Zahanati ya Nyakato.
Mwonekano wa jengo la wagonjwa katika Zahanati ya Nyakato jijini Mwanza. Kukamilika kwa jengo hili kutasaidia Zahanati ya Nyakato kupanda hadhi kuwa Kituo cha Afya na kupanua wigo wa huduma kwa wananchi hivyo wadau mbalimbali wanahimizwa kusaidia ujenzi huo ambao umeasisiwa kwa nguvu za wananchi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyakato, Mkumba.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.