LIVE STREAM ADS

Header Ads

Msanii Ben Pol ajitosa kwenye mradi wa nguruwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Msanii Ben Pol ameamua kumuunga mkono mke wa Prof. Jay katika uwekezaji wa ufugaji wa nguruwe katika mradi wa Kijiji cha Nguruwe Dodoma.

Msanii Ben Pol ametembelea mradi wa Kijiji cha Nguruwe Novemba 02,2023 ambapo amewekeza kiasi cha shilingi milioni nane huku akiwahamasisha watanzania ndani na nje ya nchi pamoja na wageni kuja kuwekeza katika mradi huo wa nguruwe.

Sambamba na uwekezaji huo msanii Ben Pol amepokea hundi ya milioni 16 kutoka kwa Mkurugenzi wa mradi huo, Grace Mgonjo ambaye ni mke wa msanii maarufu nchini na mwanasiasa Joseph Haule ‘Prof. Jay’.

Ben Pol amempongeza mke wa Prof. Jay kwa kuibua fursa hiyo adimu na kuahidi kuwaalika wasanii wenzake pamoja na wafuasi wake zaidi ya milioni 4.8 kuwekeza katika mradi huo.

Naye Dotto Ketto (Dotto Magari) amewekeza shilingi milioni 70 sambamba na kukabidhiwa hundi ya milioni 140 na Grace Mgonjo ( mke wa prof Jay ambapo anatarajia kwenda bank na bila kupitia ofisi za Piginvest International Plc kwa vile check iko tayari baada ya miezi sita.
Mke wa Prof. Jay amewaasa watanzania na watu wote duniani waje kuwekeza pesa zao ili wapate faida mara mbili ya mtaji wao baada ya miezi sita.

Nao wananchi wa Zamahero Dodoma wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji na hivyo kuvuta wawekezaji wengi na kuchochea ajira hususani kwa wanawake.

Mradi huu wa nguruwe unaenda kuweka zaidi ya shilingi Bilioni 270 ambapo njia ambayo inatumika ni njia ya Clusters au njia ya mabanda shufwa(block farming).

No comments:

Powered by Blogger.