LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya NMB yazindua kampeni ya Teleza Kigijitali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akimkabidhi simu janja na jokofu mshindi wa jumla, Paschal Saba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Novemba 08, 2023 katika viwanja vya Bombadia mjini Singida. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Singida, Alphonsina James, Meneja wa NMB Mkoa wa Singida, Emmanuel Kishosha na Meneja wa NMB, Kanda ya Kati, Janeth Shango.

Na Dotto Mwaibale, Singida
Benki ya NMB imezindua kampeni ijulikanayo Teleza Kidijitali- Weka na Ushinde ambayo inalenga kuchagiza wateja wa benki hiyo kujenga utamaduni wa kuweka fedha na akiba kwenye akaunti zao.

Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango akizungumza katika awamu ya pili ya uzinduzi wa kampeni hiyo kitaifa uliofanyika mkoani Singida Novemba 08, 2023 amesema benki hiyo imekuja na kampeni hiyo baada ya kutambua kuwa uwekaji wa akiba kwa watanzania imekuwa jambo gumu hali inayosababisha panapotokea jambo linalohitaji fedha wanalazimika kutafuta mikopo ya haraka ambayo inakuwa na riba kubwa.

"Suala la uwekaji wa akiba linazidi kuwa kubwa na sisi kama benki ya NMB inayowajali wateja wake tumeona tuje na kampeni hii ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia idadi kubwa ya wateja wetu kuwa na tabia ya kujiwekea akiba ili wasipate wakati mgumu wanapokumbana na masuala yenye udharura" amesema Shango.

Shango amesema kupitia kampeni hiyo Benki ya NMB inaendelea kuhamasisha wateja wake kutotumia akaunti zao kama sehemu tu ya kufanya miamala na kupitisha pesa bali wazitumie vyema kujiwekea akiba na kuhifadhia pesa kwani kufanya hivyo watanufaika baadae.

" Ili kurudisha faida tunayoipata kama benki kwa wateja wetu tumezindua promosheni hii itakayoshuhudia zawadi ya pesa taslimu ambayo itawekwa katika akaunti zao ili kuwahamasisha kuendelea kuwa na akiba katika aaaakaunti zao" amesema.

Kwa mujibu wa Shango amesema kampeni hiyo itakuwa na droo za kila wiki na utaratibu wa zawadi utakuwa ni kuongeza kiasi kilichopo kwenye akaunti yako kwa mara mbili kwa mshindi.

"Ni kwamba kama mteja atakuwa na Shilingi milioni moja kwenye akaunti yake na ameibuka mshindi, basi sisi NMB tutamuongezea shilingi milioni moja nyingine, tofauti na kampeni iliyopita kampeni hii tumeamua kuwa na zawadi ya aina hii ili kuhamasisha zaidi kutumia akaunti za NMB kwa ajili ya uwekaji wa akiba.

Ameongeza kuwa kampeni hii ambayo imeanza Novemba 8, 2023 itaendelea mpaka wiki ya mwezi Disemba na ni mahususi kwa wateja wote wa NMB kwa akaunti za akiba na zile za matumizi ambazo ndio za kawaida na hata kwa wale watakao jiunga na benki hiyo katika kipindi cha kampeni hii.

"NMB tutaendelea kuhamasisha matumizi ya akaunti za NMB kama njia ya kuhifadhi fedha na kujiwekea akiba ili kupata nafasi ya kushinda zawadi hizo na hivyo kufanya kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka kuwa chenye manufaa zaidi" amesema Shango.

Amesema Benki ya NMB inazohuduma bora za kidigitali ambazo zinamanufaa kwa mteja ambazo ni huduma ya mshiko faster ambayo mteja anaweza kujipatia mkopo mpaka Sh.500,000 papo hapo bila kufika kwenye tawi la benki kuweka dhamana yoyote.

Ametaja huduma nyingine inayotolewa na benki hiyo ni ya 'Spend to Save' ambayo inamuwezesha mteja kuweka akiba kwa kila tumizi lake kwenye akaunti yake na huduma ya NMB Pesa Akaunti ambayo mteja anaweza kufungua mpaka kwa Sh.1000 na tayari anakuwa na vigezo ya kujipatia huduma zingine zinazotolewa na benki hiyo.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizindua kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameishukuru Benki ya NMB kwa kuja na kampeni hiyo ambayo itatoa elimu kwa wananchi wakipata fedha zao zitakuwa salama na kuzalisha zaidi na hivyo kuchangia maendeleo ya mkoa huo.

Úwekaje wa fedha kwenye akaunti za NMB ni jambo jema na linapaswa kupokelewa kwa mikono miwili na kama unafikiri kuweka akiba sio ujanja basi kutokuweka akiba ukipatwa na tatizo utaona mziki wake na ndio utajua umuhimu wa kuweka akiba," amesema Dkt.Mganga.

Amesema suala la uwekaji akiba ni la muhimu sana katika maisha yetu kwani mara nyingi yamekuwa yakiibuka mambo ya dharura yanayohitaji fedha na unapokuwa huna akiba utaona ugumu wa kutatua tatizo husika.

Katika uzinduzi huo Benki ya NMB imetoa zawadi mbalimbali kwa washindi wenye akaunti kwenye benki hiyo ambapo mshindi namba moja Pascal Saba alizawadiwa jokofu kubwa na simu janja huku mshindi namba mbili akizawadiwa simu.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Mgoma Lake Ltd, Martin Mtinda alikabidhiwa trekta la mkopo kutoka benki hiyo lenye thamani ya shilingi milioni 27.

Amesema gharama za trkta hilo benki ya NMB imelipa asilimia 80 na mkulima atalipa asilimia 20 katika kipindi cha miaka mitatu.

Amesema alipata mkopo huo baada ya kampuni hiyo kutimiza vigezo kwa kufungua akaunti katika benki hiyo.

Kampeni hiyo ambayo imeonesha kuzaa matunda itafanyika nchi nzima kwa kuwashirikisha wateja wenye akaunti katika benki hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.Fatma Mganga akimkabidhi simu janja mshindi wa pili.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.Fatma Mganga akisoma hutuba ya uzinduzi wa kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango akiteta jambo na Meneja wa benki hiyo Mkoa wa Singida, Emmanuel Kishosha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Meneja Masoko wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Ungandeka Mwakatage, akiongoza uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.Fatma Mganga akimkabidhi ufunguo wa triketa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mgoma Lake Ltd, Martin Mtinda aliyepewa mkopo na benki hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.Fatma Mganga (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wateja wa benki hiyo waliojinyakulia zawadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.Fatma Mganga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo baada ya uzinduzi huo.

No comments:

Powered by Blogger.