LIVE STREAM ADS

Header Ads

MDH yang'ara tuzo za NBAA 2023

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
MDH imeendelea kufanya vizuri katika tuzo za Uandaaji Bora wa Hesabu ambapo kwa mwaka huu imeweza kushika nafasi ya kwanza katika Tuzo za Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) zilizofanyika Disemba 01, 2023 jijini Dar es Salaam,

"MDH imeshinda kama mshindi wa kwanza wa taarifa bora ya fedha mwaka wa 2022 katika kitengo cha mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoripoti kwa kutumia IPSAS. Tuzo hii imetolewa na Bodi ya Kitaifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye Kongamano la Mwaka la 2023 la NBAA".

"Kwa miaka miwili mfululizo (2020 na 2021) MDH imekuwa mshindi wa pili kwenye kitengo kimoja. Tuzo hii inaonyesha uaminifu, uwajibikaji na uwazi kwa serikali, washirika, wakiwemo wafadhili wetu na watu tunaowahudumia" amesema CPA. Damasco Peter, Mkurugenzi wa Fedha MDH.

No comments:

Powered by Blogger.