LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jeshi la Polisi Mwanza laadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza limeungana na wadau mbalimbali kuadhimisha kampeni ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10.

Maadhimisho hayo yamefanyika Ijumaa Disemba Mosi 2023 katika uwanja wa polisi mabatini huku rai ikitolewa kwa jamii na wadau kushirikiana ili kuimarisha malezi bora kwa watoto hatua itakayosaidia kukabiliana na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Askari wa jeshi la polisi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Askari wa jeshi la polisi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Watoto wakitoa burudani ya ngoma ya asili.
Viongozi mbalimbali meza kuu wakishuhudia burudani ya ngoma.
Washiriki wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.