LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya NMB Kanda ya Ziwa yasherehekea Uhuru wa Tanzania Bara kwa bonanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya NMB Mkoa wa Geita imefanya vizuri katika mashindano ya bonanza la michezo la benki hiyo yaliyofanyika katika shule ya sekondari Chato wilayani Chato ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika/ Tanzania Bara.

Katika bonanza hilo, NMB Geita imefanikiwa kushinda katika mchezo wa kuvuta kamba kwa upande wa wanaume dhidi ya benki ya NMB Kagera. Kwa upande wa mpira wa wavu NMB Geita imeibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya NMB Kagera. Katika mchezo wa mpira wa pete, NMB Geita imeshinda kwa mabao 10-1 dhidi ya NMB Kagera.

Kwa upande wa mpira wa miguu, NMB Kagera imeshinda kwa mabao 3-0 dhidi ya NMB Geita. Mabao ya NMB Kagera yamefungwa na Dastan Kato katika dakika ya 16, Aidan Mshua katika dakika ya 34 na Gosbert Madembwe katika dakika ya 85.

Meneja wa timu ya NMB Geita, Derick Kamugisha ameipongeza timu yake kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali. Kamugisha amesema watajipanga vizuri zaidi kwa jili ya bonanza lijalo.

Meneja wa timu ya NMB Kagera, Aidan Kanyari amesema bonanza hilo limewasaidia katika kuendeleza umoja kupitia michezo baina ya wafanyakazi wa NMB Geita na NMB Kagera. Ameuomba uongozi wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa, bonanza hilo liwe endelevu.

Naye Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Wogofya Mfalamagoha amewapongeza wafanyakazi wa benki hiyo kutoka mikoa ya Kagera na Geita kwa kushiriki katika bonanza hilo.

Amesema wafanyakazi wa benki ya NMB wanatakiwa kuandaa timu za mikoa kupitia matawi yao kisha kuandaa timu ya Kanda itakayokuwa imara kwa jili ya kushindana na Kanda nyingine za benki hiyo.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.