LIVE STREAM ADS

Header Ads

Miaka 62 ya Uhuru, Mwanza wapiga hatua

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ameshiriki mdahalo wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika/ Tanzania Bara uliolenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo maendeleo ya Mwanza tangu uhuru.

Mdahalo huo umefanyika Jumamosi Desemba 09, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini, watumishi, wanafunzi wa sekondari, wanachuo, wanasiasa na wakufunzi kutoka Chuo cha SAUT.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Makilagi MEsema katika miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika,  Mkoa wa Mwanza umepata maendeleo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu na miundombinu ya barabara.

"Kwenye upande wa elimu Mkoa wa Mwanza kabla ya uhuru tulikuwa na shule tano za sekondari ikiwemo shule ya wavulana Bwiru iliyojengwa mwaka 1920 na ya wasichana iliyojengwa mwaka 1952 lakini hadi sasa Mkoa wetu wa Mwanza tuna shule 332 na watoto wanasoma bila ubaguzi ukilinganisha na zamani" amesema Makilagi.

Akizungumza miundombinu ya barabara Makilagi amesema kabla ya uhuru Mkoa wa Mwanza ulikuwa na kilometa za rami 8.81 lakini hadi sasa kuna kilometa 359,000, barabara za changalawe zilikuwa kilometa 1,961 mara baada ya uhuru kupatikana sasa hivi kinakilometa 2,213.

Aidha amesema kuwa hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja unazidi kuimarika kutokana na uhuru uliopo wa watu kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ukilinganisha na zamani kabla ya uhuru ambapo watu walikuwa hawana uhakika wa kula.

Akiwasilisha mada ya uchumi katika mdahalo huo, Mhadhiri wa Biashara kutoka Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Dkt.Ntui Ponsian amesema Serikali inatakiwa iboreshe sekta binafsi kwani ndio waajiri wakubwa wa vijana hapa nchini hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Askofu Denis Nkwera kutoka Umoja wa Makanisa ya CPCT amesema kabla ya uhuru kulikuwepo na ubaguzi mkubwa wa dini lakini hivi sasa ubaguzi huo haupo watu wanashurikiana vizuri katika kuilinda tunu ya amani iliyowekwa na Mungu.

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Geofrey Kavenga amesema hali ya siasa imeimarika kutoka kwenye mfumo wa chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi vya siasa ikiwa ni ishara ya kuwa na siasa safi.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makala kwenye maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika/ Tanzania Bara uliopatikana Disemba 09, 1961.
Muhadhiri wa Biashara kutoka SAUT Dkt.Ntui Ponsian akitoa mada ya uchumi kwenye mdahalo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru.
Mmoja wa washiriki akichangia hoja kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wakiwemo viongozi wa dini wakifuatilia mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru uliofanyika Disemba 09, 2023 jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.