Mwekezaji wa nguruwe agawa tiketi kwa mashabiki wa soka
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa mradi wa Kijiji cha Nguruwe uliopo mkoani Dodoma, Simon Mnkondya amegawa bure tiketi 100 kwa mashabiki wa soka kwa ajili ya kushuhudia mchezo kati ya Simba SC na Dodoma Jiji utakaofanyika Ijumaa Mei 17,2024 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mkurugenzi huyoa maarufu kama Mr. Manguruwe ambaye ni shabiki kindakindaki wa Simba amegawa tiketi hizo katika soko la Machinga Complex Dodoma.
"Katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua michezo nchini kama ilivyo kwa Rais wa serikali ya Jamhuri ya mlmuungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akinunua magoli katika vilabu vya Simba SC na Yanga, nimegawa tiketi 100 kwa mashabiki kuelekea mechi ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba SC mchezo utakaopigwa katika uwanja vya Jamhuri Dodoma" amesema Mr. Manguruwe.
No comments: