LIVE STREAM ADS

Header Ads

CGP. Nyamka awavisha nishani maafisa magereza Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP. Mzee Ramadhan Nyamka amewavisha nishani mbalimbali maafisa 279 wa jeshi hilo kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Maafisa hao ni miongoni mwa maafisa 2263 Tanzania Bara waliotunukiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nishani ya miaka 60 ya Muungano, nishani ya utumishi uliotukuka, nishani ya utumishi mrefu na nishani ya utumishi mrefu na tabia njema.

Hafla ya kuwavisha nishani hizo imefanyika Alhamisi Mei 23,2024 katika uwanja wa gereza la Butimba jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.