LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Fedha Jiji la Mwanza yataka miradi ikamilike kwa wakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, imekagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuagiza miradi hiyo kukamilika kwa wakati.

Kamati hiyo ikiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha imefanya ziara ya kukagua miradi hiyo Ijumaa Mei 24, 2024 ambapo miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa barabara ya Buhongwa- Igoma, soko kuu jijini Mwanza.

Miradi mingine ni mabweni mawili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhongwa, vyumba vitano vya madarasa shule ya msingi Bulale na vyumba 10 vya madarasa shule ya msingi Nyerere Igoma.

Katika ujenzi wa barabara ya Buhongwa- Igoma yenye urefu wa kilomita 14 inayojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 22, Kotecha amemtaka mkandarasi kampuni ya Zhongmei Group kuongeza kasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati kwani ni tegemeo kwa wananchi.

"Mkataba wa mradi huu ulianza mwezi Septemba 2023 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Februari 2025. Muda uliobaki ni kidogo kwa hizi asilimia 14 mnazosema mmefikia, ongezeni kasi" alishauri Kotecha.

Katika ujenzi wa soko kuu jijini Mwanza, mradi umefikia asilimia 94 ambapo Kamati ilishauri Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kufuatilia kwa ukaribu utoaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ili kuondoa adha iliyopo kwa wafanyabiashara na wananchi.

Kamati pia ililidhishwa na ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wenye mahitaji katika shule ya msingi Buhongwa yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 160 ambayo ujenzi wake umegharibu shulingi milioni 320 pamoja na samani zake.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (kulia) akiteta jambo na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Mwonekano wa baadhi ya vyumba vya madara katika shule ya msingi Nyerere iliyopo Kata ya Igoma. Serikali imetoa shilingi milioni 270 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 vya madara na ofisi ya waalimu.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Nyerere iliyopo Kata ya Igoma ukiendelea.
Mwonekano wa moja ya bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Buhongwa iliyopo Kata ya Igoma.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakikagua ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya msingi Buhongwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Jiji la Mwanza akishuhudia samani zilizowekwa kwenye bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buhongwa.
Mwonekano wa ndani wa vyumba katika bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Buhongwa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakikagua ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya msingi Buhongwa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakikagua ujenzi wa vyumba vitano vya madara na ofisi ya waalimu katika shule ya msingi Bulale iliyopo Kata ya Bulale.
Mwonekano wa ujenzi wa barabara ya Buhongwa- Igoma inayojengwa kwa kiwango cha lami.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.