LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hoteli mpya yafunguliwa Tinde Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amezindua hoteli mpya 'AZAT HOTEL' iliyopo katika kata ya Tinde wilayani Shinyanga .

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika Juni 01, 2024 katika viwanja vya hoteli ya AZAT HOTEL vilivyopo jirani na kituo cha mzani wa Tinde wilayani Shinyanga.

Awali mmiliki wa hoteli hiyo, Azza Hamad amewakaribisha wateja kwenda kujipatia huduma bora zinazotolewa hotelini hapo.
"AZAT Hoteli ni sehemu sahihi kwa ajili ya kupumzika kwa wageni na hata wenyeji, huduma zitakazotolewa hapa AZAT HOTEL ni pamoja na malazi na chakula kwa gharama nafuu" amesema Hamad.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amepongeza uwekezaji uliofanywa na Azza Hamad kwa kuthamini wageni na kuongeza mapato, uchumi na maendeleo kwenye halmashauri hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana vyema na wawekezaji.
"Hongera sana dada yetu Azza Hamad kwa uwekezaji uliyoufanya kwenye Kata hii ya Tinde ukizingatia ni miongoni mwa maeneo yanayopokea wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali" amesema Mtatiro.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude amesema hoteli hiyo itatoa fursa ya ajira na kuwasihi kufanya kazi kwa bidii huku akitoa wito kwa jamii kushirikiana vyema na wawekezaji ili kuwatia moyo waendelee kuwekeza kwenye maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Zoezi la kukata utepe kuashiria uzinduzi kwenye hoteli ya AZAT Hotel.
Muonekano wa ndani hoteli ya AZAT Hoteli.
Muonekano wa nje hoteli ya AZAT Hotel.
Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa hotel ya AZAT Hoteli.

No comments:

Powered by Blogger.