LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyabishara soko la Mbugani watakiwa kuwa wavumilivu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wafanyabiashara katika soko la Mbugani jijini Mwanza, wametakiwa kuwa wavumilivu wakati ujenzi wa soko Kuu Mjini Kati ukitarajiwa kukamili na kutoa fursa ya wao kurejea katika soko hilo.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Hamad Nchola alitoa rai hiyo Mei 30, 2024 wakati akizungumzia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara sokoni hapo tangu wapishe ujenzi wa soko kuu.

“Soko hili lina changamoto hili, lakini kama tunavyojua tulihamia hapa kwa muda ili kupisha ujenzi wa soko kuu mjini kati hivyo niwaombe wafanyabiashara waendelee kuwa watulivu kwani ujenzi umefikia asilimia 94” alisema Nchola.

Nchola alitoa rai kwa Serikali kuongeza kasi ya ujenzi wa soko kuu jijini Mwanza kwani muda wa miaka miwili uliopangwa umeisha na sasa ni mwaka wa nne hivyo ni vyema likakamilika na kuanza kutumika ili kuondoa adha iliyopo.

Awali baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mbugani akiwemo Sophia Nyema na Steven Nigula walisema soko hilo linakabiliwa na ubovu wa miundombinu hasa wakati wa mvua ambapo baadhi ya maeneo huvuja na kuathiri bidhaa zao.

“Walituambia tuhamie hapa, wataporesha miundombinu lakini mpaka sasa hali ni mbaya, mvua ikinyesha hapa panakuwa kama Ziwa kiasi kwamba hata wateja hawaji. Tunaomba wakamilishe hilo soko kuu la mjini kati ili turejee kule” alisema Nyema.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.