Spika wa Bunge afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA.
Aidha Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujali maslahi ya watanzania.
Pamoja na hayo Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.
No comments: