LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Nyamagana achangia uboreshaji sekta ya elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula ameendelea kusaidia uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awamu hii ametimiza ahadi yake katika Kata ya Pamba kwa kuchangia madawati 100 kwa ajili ya Shule za Sekondari Mlimani na Bugarika.

Akikabidi madawati hayo Jumatano Julai 10, 2024, Mabula alisema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga vyumba vya madarasa ikiwemo majengo ya ghorofa katika shule mbalimbali jimboni humo hivyo ofisi ya mbunge itaendelea kuunga mkono jitihada hizo.

"Mwaka huu wa fedha (2024/25) tumetenga shilingi milioni 30 kwa ajili ya madawati ya wanafunzi, viti na meza kwa ajili ya waalimu. Kupitia fedha za Serikali Kuu, mapato ya Halmashauri na fedha za mfuko wa jimbo tutaendelea kuboresha zaidi sekta ya elimu" alisema Mabula.

Baadhi ya wanafunzi katika shule za sekondari Mlimani na Mbugani zilizopo Kata ya Pamba, walisema kumekuwa na adha ya uhaba wa madawati katika shule hizo hiyo mchango wa madawati hayo utasaidia kupunguza adha iliyokuwepo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akikaidhi madawai katika shule ya sekondari Bugarika jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kulia) akikaidhi mipira kwa ajili ya wanafunzi shule ya sekondari Bugarika.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akikabidhi madawati katika shule ya sekondari Mlimani jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.