LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI lafungua ofisi mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la jijini Mwanza, limefungua ofisi kubwa na ya kisasa mjini Shinyanga, ili kuimarisha shughuli za utekelezaji wa miradi ya NOURISH na GROW ENRICH katika wilaya za Shinyanga na Kishapu.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Yassin Ally amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2023 hadi 2027 kwa ufadhili wa shirika la World Vision kupita Serikali za Ujerumani na Ireland.

"Miradi hii inalenga kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma za lishe, afya ya mama na mtoto na afya ya uzazi kwa vijana" amesema Meneja Miradi shirika la KIVULINI, Eunice Mayengela.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja Miradi shirika la KIVULINI, Eunice Mayengela akiwa ofisini mjini Shinyanga.
Afisa wa shirika la KIVULINI akiendelea na majukumu katika ofisi ya shirika hilo mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa shirika la KIVULINI wakiendelea na majukumu katika ofisi ya shirika hilo tawi la Shinyanga.
Wafanyakazi wa shirika la KIVULINI wakiendelea kutimiza majukumu yao mjini Shinyanga.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.