Mchungaji Ezekiel Odero kuunguruma Mwanza "injili si maneno, ni vitendo"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mratibu wa kongamano la injili lililoandaliwa na kanisa la New Life Prayer Center la Mombasa nchini Kenya, Nabii Utukufu kwa Bwana amesema injili ya Yesu Kristo siyo maneno yanayohubiriwa mdomoni bali ni vitendo halisi vinavyogusa maisha ya mwanadamu.
Alibainisha hayo Julai 22, 2024 katika uwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza litakapofanyika kongamano hilo kuanzia Julai 24- 28, 2024 likiongozwa na Mchungaji Ezekiel Odero.
Nabii Utukufu alieleza kuwa moja ya malengo ya mkutano huyo ni kuliombea amani Taifa la Tanzania pamoja na uponyaji utakaoambatana katika maisha ya watanzia.
"Tuliandaa mikutano mikubwa Arusha, Dar es salaam na Morogoro ambapo watu walipokea uponyaji mkubwa, tukaona ni vyema tukafika Mwanza ili watu pia wafunguliwe" alisema Nabii Utukufu.
Nao baadhi ya waumini wa kanisa hilo walieleza kuwa kupitia kongamano hilo, wanatumaini kupata miujiza na uponyaji wa magonjwa mbalimbali yanayowasumbua kwa muda mrefu.
"Tuwakaribishe watu mbalimbali kuhudhulia kongamano hili kubwa ambapo kwa imano tutapokea uponyaji wetu" walisema.
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
Na Chausiku Said, Mwanza
No comments: