LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi Zanzibar wafanya ziara Shirika la KIVULINI Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wamefanya ziara ya kimafunzo katika shirika la KIVULINI lililopo jijini Mwanza ili kujifunza mbinu zaidi za kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ziara hiyo ya siku tatu imeanza Jumatano Julai 03, 2024 ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Abeida Rashid Abdallah aliyeeleza kuvutiwa na mbinu za shirika la KIVULINI katika kutoa elimu ya kuzuia ukatili.

Mratibu wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake visiwani Zanzibar, Ali Wadi Ame amesema mbinu bora za shirika la KIVULINI zimewavutia kufika katika shirika hilo ili kujifunza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto na wanawake, Yassin Ally amesema shirika hilo limekuwa likitumia mbinu ya SASA ili kufikia makundi mbalimbali katika jamii hivyo kama mbinu hiyo itatumika Zanzibar italeta pia matokeo makubwa.

Ujumbe wa viongozi hao kutoka Zanzibar utakutana na makundi mbalimbali katika jamii ili kujifunza zaidi kuhusu mbinu za kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanyakazi wa shirika la KIVULINI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Abeida Rashid Abdallah (katikati) akizungumza wakati wa ziara ya kimafunzo katika shirika la KIVULINI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada wakati wa ziara ya kimafunzo ya viongozi kutoka Zanzibar.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.