LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana wahimizwa kuchangamkia fursa za zabuni PPRA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imewahimiza vijana kusajili vikundi na makampuni ili kupata sifa ya kuomba tenda na zabuni mbalimbali zinazotangazwa na mamlaka hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Kwame Simba ametoa rai hiyo Jumapili Oktoba 13, 2024 alipotembelea maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika kitaifa jijini Mwanza kuanzia Oktoba 08- 14, 2024.

Simba amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fursa kwa vijana kushiriki zabuni mbalimbali zenye thamani hadi shilingi bilioni 50 hivyo vijana wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.

PPRA ni miongoni mwa taasisi na mashirika mbalimbali yaliyoshiriki kwenye maonesho ya wiki ya vijana kitaifa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, ili kutoa elimu kwa wananchi ambapo maadhimisho hayo yameambatana na kaulimbiu isemayo “vijana na matumizi ya fursa za kidigitali kwa maendeleo endelevu”.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Kwame Simba akizungumza na wanahabari kwenye maaonesho ya wiki ya vijana kitaifa jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Kwame Simba akisaini kitabu alipotembelea banda la Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGa).
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Kwame akiteta jambo kwenye banda la jeshi la polisi.
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Kwame akizungumza na wanahabari namna mamlaka hiyo inatoa fursa kwa vijana kushindania zabuni mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.