Rais Samia atoa ajira 4,000 za waalimu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuajiri walimu wa somo la biashara 4,000 kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Walimu hao watafuata mtaala mpya unaotumika, unaolenga kuleta mapinduzi ya elimu nchini kwa kuimarisha elimu ya biashara kwa wanafunzi.
Akifungua Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Udhibiti ubora wa Wilaya Wateule Novemba 23,2024 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema walimu hao watafundisha elimu ya biashara kuanzia mwakani.
#KaziInaongea
No comments: