Serikali ya Rais Samia kujenga kizazi chenye kufikiri
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Novemba 22,2024 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ili kufanikisha hatua hiyo serikali imeamua somo la biashara litakuwa ni lazima kwa wanafunzi wote kuanzia mwaka wa masomo 2025/26 ili kujenga kizazi chenye kufikiri kwa mlengo wa kibiashara.
Mbali na hilo, Majaliwa ameviagiza vyuo vya biashara kufanya mapitio ya mitalaa yao ili kujenga tabia ya vijana wanaohitimu, kupenda kubuni na kufanya biashara badala ya kusubiria kuajiriwa serikalini ambapo nafasi zimejaa na wengi wana umri wa miaka 30.
Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la tano la maendeleo ya biashara na uchumi, lililoandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) tawi la Dodoma.
“Serikali kwa upande wetu, kupitia Sera ya mafunzo ya mwaka 2023, tunaelekeza somo la biashara liwe la lazima kwa wanafunzi wote kuanzia mwaka wa masomo 2025/2026 na kuendelea” amesema Majaliwa.
#KaziInaongea
No comments: