LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wenje asaka kura za CHADEMA Mwanza, Geita na Mara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Joto la kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji limeendelea katika maeneo mbalimbali nchini huku vyama vya siasa vikiendelea kuwanadi wagombea wao kwa wananchi ili wapigiwe kura Novemba 27, 2024.

Huko mkoani Mara katika Wilaya ya Rorya, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje amefanya mikutano katika Vijiji mblimbali zaidi ya sita.

Wenje amefanya mikutano ya kampeni katika Kijiji cha Mkengwa Kata ya Nyamunga, Kijiji cha Makongoro Kata ya Rabuor, Kijiji cha Ikoma Kata ya Ikoma, Kijiji cha Nyamasanda Kata ya Namasanda, Kijiji cha Panyako Kata ya Gobire na Kijiji cha Sakawa Kata ya Kitembe.

Mbali na Rorya mkoani Mara, Pia Wenje ameiga mikutano jijini Mwanza katika Kata za Mabatini, Butimba, Mkolani, Kishiri na Igoma pamoja na Katoro mkoani Geita.

Katika mikutano hiyo ya kuwanadi wagombea wa CHADEMA, Wenje ametoa rai kwa wananchi kukipa nafasi chama hicho kwa kuwapigia kura za ndiyo wagombea wake kwa manufaa ya maendeleo yao huku ahadi yao ikiwa ni kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo michango na tozo zisizo na tija kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje akiwaombea kura wagombea wa chama hicho kwenye kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje akiwa na makada mbalimbali wa chama hicho kwenye kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje akiwa na viongozi pamoja na makada mbalimbali wa chama hicho kwenye kusaka kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje akizunugumza kwenye mkutano wa kampeni wilayani Rorya.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.