Biteko ataka walalamishi wasipigiwe kura
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi wamehimizwa kufuatilia kampeni za Uchauzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini lakini wasifanye makosa kuchagua viongozi wa upinzaji kwani wamekosa agenda na badala yake wamekalia kulalamika.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo wakati akiwanadi wagombea wa chama hicho katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Aidha Dkt. Biteko akiwa katika jimbo lake la Bukombe mkoani Geita, ametoa rai kwa wananchi na hasa wana CCM kuhakikisha wanabeba kura zote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 na hata Uchaguzi Mkuu ujao mwakani 2025.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: