CHADEMA Mwanza wazindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Miaa, Vitongoji na Vijiji unaotarajia kufanyika nchini Noemba 27, 2024.
Kote nchini, kampeni hizo zilianza Novemba 20, 2024 zikitarajiwa kufikia tamati Novemba 26, 2024 ambapo kwa Mkoa Mwanza CHADEMA wamefanya uzinduzi rasmi Ijumaa Novemba 22, 2024 katika eneo la Mabatini jijini Mwanza.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ambaye amewahimiza wanachama wa chama hicho kujitokeza kuwapigia kura wagombea wao ili kuhakikisha wanashinda.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu akizungumza katika uwanja wa shule ya msingi Mabatini jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
Tazama BMG TV LIVE hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: