LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kishindo cha Rais Samia sekta ya umeme

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkakati wa kukuza uchumi kwa nchi na wananchi wa Tanzania unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan umeleta tija kubwa katika sekta ya umeme nchini.

Tangu aingie madarakani Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia sekta muhimu na za kimkakati kwa lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ameweza kuimarisha upatikanaji wa umeme vijijini kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA),sasa vijiji vingi vina umeme kwa mara ya kwanza, huku gharama za kuunganishwa zikipunguzwa kwa ruzuku.

Kama haitoshi amesimamia miradi mikubwa ya kuzalisha umeme kwa kuendeleza mradi wa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) ambao utaongeza megawati 2,115 kwenye gridi ya taifa.

Aidha kumekuwa na vyanzo vya nishati mseto kama jua, upepo, na makaa ya mawe pia vinaendelezwa.

Rais Dkt. Samia ameboresha usambazaji wa umeme wa uhakika hatua inayowezesha shughuli za kiuchumi, elimu, afya, na biashara kwa kiwango bora zaidi.

Katika kipindi cha miaka minne kumekuwa na mikataba ya kizalendo, ambapo kumalizika kwa mkataba wa Songas kumeipa serikali udhibiti zaidi wa sekta ya umeme, ikilenga kupunguza gharama na kuboresha huduma kwa wananchi.

Haya yote ni msingi wa kufanikisha lengo la Tanzania kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025, huku wananchi wakifaidika kwa umeme wa gharama nafuu na uhakika.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.