LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia na maono ya kuifanya Tanzania ya Kilimo cha Umwagiliaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maono ya Serikali ya awamu ya sita, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwekeza kwenye Kilimo cha Umwagiliaji ambapo amedhamiria kuwekeza katika Kilimo hicho na kujipanga ifikapo mwaka 2030, asilimia 50 ya Kilimo cha Tanzania kuwa cha umwagiliaji.

Katika jitihada hizo za Rais Dkt. Samia katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, anaendelea kutekeleza miradi mipya ya Kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 543,366 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.18.

Rais ameuelezea mpango huo wa Serikali kuwa ni kuendeleza utoshelevu wa chakula na utekelezaji wa dhana ya Kilimo Biashara.

Serikali imeamua kuwekeza katika kilimo hicho cha Umwagiliaji na imejipanga ifikapo mwaka 2030, asilimia 50 ya kilimo cha Tanzania kiwe cha umwagiliaji ili kuwa na kilimo cha biashara zaidi.

Rais Dkt. Samia ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa una Miradi 33 ya umwagiliaji inayojumuisha Ujenzi, Ukarabati, Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika skimu mabwawa na mabonde yenye thamani ya Shilingi Trilioni 32.4.

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, ametoa ufafanuzi kuhusu Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Tanzania uliofanyika hivi karibuni nchini China na kusema kuwa, Rais Dkt.Samia ametoa agizo kwa wakulima nchini kuanza kulima kwa kutegemea maji ya kumwagilia badala ya mvua.

Kauli hiyo ya Rais inahusu mkakati wa kukuza kilimo cha kisasa, ambapo Wizara ya Kilimo imepewa jukumu la kujenga mabwawa na kuvuna maji ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinafanikiwa na kwamba China imetenga kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 360 kwa Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Sehemu ya fedha hizi itaelekezwa moja kwa moja kwenye sekta ya umwagiliaji nchini Tanzania, ambapo mradi huo unatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa wakulima na katika kipindi hicho, serikali itahakikisha kuwa miradi yote ya umwagiliaji iliyopo itakamilishwa na miradi mipya itaanzishwa ili kuwasaidia wakulima kote nchini.

Mkakati huu wa Serikali hii yenye maono ya mbali, una lengo la kuleta Mapinduzi katika Sekta ya Umwagiliaji, hivyo miradi yote aliyoahidi katika mradi huo itatekelezwa.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.