Rais Samia atoa Bilioni 24 Namtumbo Ruvuma
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com Katika jitihada zake za kuleta maendeleo nchini, Serikali ya Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Huu ni muendelezo wa mikakati ya Rais Dkt. Samia tangu alipoingia madarakani, ambapo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 24 kwa kutekeleza miradi ya maendeleo Namtumbo.
Miradi iliyohusishwa katika fedha hizo ni ujenzi wa Shule ya Wasichana, Miradi ya kusambaza umeme kwenye vijiji na vitongoji, elimu, afya, kilimo, maji,ujenzi wa kituo cha Polisi na Mahakama katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amempongeza Rais Dkt. Samia kwa jitihada zake alizofanya katika kipindi miaka mitatu tangu kuingia madarakani, ambapo katika Sekta ya umeme, vijiji zaidi ya 12,000 Tanzania Bara, vimepata umeme na kazi hiyo imefanyika kwa mafanikio.
Katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilayani Namtumbo, Kapinga amewataka viongozi watakao chaguliwa katika ngazi za mitaa, vijiji na vitongoji wawatumie Wananchi ipasavyo, pia watoe huduma bora na kusimamia maelekezo ya Serikali ikiwemo kampeni ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Kampeni hiyo inayohamasishwa na Mama Samia, kwa kuanzia katika Wilaya hiyo, imefunga jiko la kisasa la kupikia katika shule mpya ya sekondari ya wasichana Namtumbo.
#KaziInaongea
No comments: