Mabula akabidhi Tuzo za Filamu Nyamagana 2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto) akikabidhi tuzo ya mwigizaji bora wa kiume kwenye tuzo za Nyamagana Film Awards 2024 zilizoandaliwa na ofisi ya Mbunge Nyamagana kwa kushirikiana na chama cha waigizaji wa filamu Wilaya ya Nyamagana, Ijumaa Novemba 22, 2024.
MBUNGE MABULA AWEKA HISTORIA MPYA NYAMAGANA, UANDAAJI WA TUZO ZA UIGIZAJI.
Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameweka historia mpya Mkoani Mwanza kwa kuandaa tuzo kwa wasanii wa uigizaji Wilayani Nyamagana zijulikanazo kama Nyamagana Film Award 2024.
Tuzo hii ina dhima ya kuinua sanaa ya uigizaji nchini ili kuwatia Moyo na kuwajengea uwezo waandaji wa Filamu bora zitakazo kidhi soko la ushindani ndani na nje ya Tanzania kwa kuwatunuku wasanii, waandaaji pamoja na wasambazaji.
Mhe. Mabula amesema, idadi kubwa ya watu waliohudhulia hafla ya utoaji tuzo kwa msimu wa kwanza 2024 ni ushawishi tosha kuongeza nguvu ya uboreshaji uandaaji wa Nyamagana Film Awards msimu wa pili 2025 kwa ubora zaidi
Ikiwemo kuongeza idadi ya washiriki, uandaaji katika ukumbi mkubwa, kuongeza idadi ya wadhamini na zawadi ili kuipa thamani tuzo hizo. Kadharika ametumia adhra hiyo, kuwahakikishia wasanii kuleta mapinduzi katika sekta ya Filamu ikiwemo kutumia sanaa kutangaza Nyamagana.
Mhe. Mabula akijibu risala ya Chama Cha Waigizaji Nyamagana, Mhe. Mabula amekubali kufadhiri Filamu itakayobeba maaudhui yenye vionjo vya mira, desturi, tamaduni na Utalii wa Nyamagana ambayo itazinduliwa rasmi 2024.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana- Thomas Salala akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya Bi. Amina Makilagi amempongeza Mhe. Mabula kwa jitihada zake za kuiinua sanaa Nyamagana na kumhaidi ofisi yake kushirikiana na Halmashauri Jiji la Mwanza kuweka mazingira wezeshi kwa wasanii hao kunufaika na mikopo ya 10% ya mapato ya Halmashauri.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza- Mhe. Sima Costantine amesema, Mhe. Mabula nikiongozi mwenye maono anathamini watu wanaomzunguka hivyo uandaaji wa Tuzo hizo ni kielelezo tosha cha dhamira aliyoyonayo katika kuwatumikia wana Nyamagana.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Filamu Wilaya ya Nyamagana- Sakum Abdallah akisoma risala kwa mgeni rasmi amesema, Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amefadhili Tuzo hizo kwa 99% hivyo amemuomba kwa mwaka 2025 kuendelea kufadhili Tuzo hizo sanjari na uandaaji wa Film ya itakayo Tangaza Utalii wa Nyamagana kwa kushirikiana na msanii mkongwe nchini Gabo katika hafla ya Nyamagana Film Awards 2024.
Mgeni maalum katika hfla hiyo Mwigizaji Mkongwe wa Filamu nchini Ndg. Gabo Zigamba amesema, amemfahamu Mbunge Mabula kabla hajawa na jina kubwa, na miongoni mwa watu waliomshika mkono hadi kufanikiwa katika tasnia ya Filamu. Hivyo wana Nyamagana wanayo bahati kubwa kuwa na kiongozi anayethamini sanaa na kuwapenda wasanii.
Naye Mjumbe Baraza la Kuu Umoja wa Wanawake Tanzania ambaye pia ni Katibu Jimbo La Nyamagana Bi. Florah Magabe amesema, anamefanya kazi na Mhe. Mabula zaidi ya Miaka 8, na miongoni mwa vitu ambavyo Mhe. Mabula amevipa kipaumbele ni jinsi gani atawawezesha na kuwajengea uwezo wasanii watumie sanaa yao kama ajira ili kuzalisha matajiri (Millioner na Billioners) wengi katika wilaya ya Nyamagana kupitia sanaa.
Tuzo za Filamu Nyamagana 2024 zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali, wasanii, Afisa Michezo Mwanza Jiji, Bitegeko na Afisa utamaduni Mwanza Jiji, Bi. Majinge. Na kuandaliwa na Ofisi ya Mbunge Nyamagana kushirikiana na ofisi ya Utamaduni Jiji la Mwanza, Chama cha waigizaji wa filamu Wilaya ya Nyamagana pamoja na VOT na kupambwa na Burudani ya Kwaya, Ngoma pamoja na Muziki wa kizazi kipya.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo La Nyamagana🇹🇿
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: