Rais Samia asifu amani na utulivu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesifu amani na utulivu uliokuwepo katika zoezi la kupiga kura kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa nchini.
Watanzania wamepiga kura kwa amani hivyo ni vyema matokeo yatangazwe kwa usawa na amani, kama yatakavyokuwa yamejionyesha kwenye masanduku ya kura.
“Naomba amani hii ielendelee mpaka zoezi la kupiga kura litakapokamilika sambamba na zoezi la kuhesabu kura nalo lifanyike kwa amani na utulivu” amesema Rais Samia.
Katika kuonyesha kutotaka kuvunjika kwa amani, Rais Samia ameongeza kuwa, kura hizi ni mtindo wetu wa Demokrasia, utamaduni wetu wa Kisiasa, hivyo wahesabu kura waende wakafanye zoezi hilo kwa kwa usalama na amani.
Wapiga kura wametakiwa kuendelea na zoezi hilo kwa maelewano, na kwamba anatumaini siku hii itaenda vizuri na pia ana matumaini watawachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na pia Viongozi na Wasimamizi wa Uchaguzi, anapaswa kusimamia Uchaguzi huo kwa haki, lli kudumisha amani ya Taifa.
#KaziInaongea
No comments: