Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wafanyika kwa amani
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Usawa katika majukwaa ya kisiasa kwa vyama vyote uliotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeonekana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaoendelea, ambapo kumekuwa na utulivu katika maeneo yote ya nchi.
Hatua hiyo imeifanya Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa kuweka wazi kuwa uchaguzi huo unakwenda katika hali ya amani na utulivu.
Jumatano Novemba 27, 2024, Waziri Mchengerwa amekuwa miongoni mwa Watanzania walioitumia VEMA haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura katika kituo chake alichojiandikishia cha Umwe Mchikichini kilichopo Ikwiriri Jimboni kwake Rufiji Mkoa wa Pwani, Waziri Mchengerwa amesema taarifa alizonazo mpaka sasa uchaguzi unaendelea kwa hali ya amani na utulivu nchi nzima.
#KaziInaongea
No comments: